moja ya vyura wa kihansi waliorudi kutoka nchini Marekani.


Kaka Ankal,

Ninafuraha kuwafahamisha wadau na wa TZ kwa ujumla kuwa wale vyura 100 waliorudishwa toka Marekani na kutunzwa katika maabara maalum (Kihans sray toad captive facility) iliyopo Chuo Kikuu (UDSM) wameongezeka baada ya vyura wanane kuzaa vitoto nane. Kwa hiyo sasa wapo vyura 108 maana hamna aliyekufa.

Tuendelee kuwaombea waishi vyema hata watakaporudishwa kwenye makazi yao ya asili ili tuweze kurudishiwa urithi wetu wote toka USA.

Ni mimi Jackson mdau toka UDSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. wana faida gani?

    ReplyDelete
  2. Nafurahi kusikia hivyo..ila sijui km hawa watu hawajawadunga madawa yao maana..

    ReplyDelete
  3. Kama wa-Tanzania wengine, nimefuatilia kwa karibu habari ya vyura wetu hao, tangu mwanzo. Nimekuwa na suali ambalo labda kuna wanaoweza kujibu.

    Tuliruhusu vyura wetu hao kusafirishwa Marekani, ambako walikaa miezi mingi. Na sasa tunaambiwa wamerudi tena chini. Je, walipokuwa huko Marekani, sisi tulikuwa na ufuatiliaji gani wa kujua kama wamezaliana au la. Na kama wamezaliana, tumerudishiwa pia vitoto vya hao vyura?

    Suali hili limeitatiza akili yangu muda wote huo, maana naogopa isije ikawa tumeingizwa mjini, halafu vyura wetu wengine wakawa bado huku ughaibuni, wakati ilijulikana kuwa sehemu yenye vyura hao ni Kihansi tu. Naomba ufafanuzi, na nitashukuru.

    Hili suali linanitatiza kwa sababu zama zetu hizi kuna tatizo kubwa la uporwaji wa mali asili kama vile wanyama, mimea, kama vile mimea ambayo inatoa dawa, na kadhalika. Ni tatizo kubwa duniani.

    ReplyDelete
  4. vyura wanazaa au wanataga

    ReplyDelete
  5. Ujue Marekani wanakula chura, ndo maana wanaangaika sana kuwaokoa. Tena mimi ninalo gazeti lililoandikwa kuhusu taafifa ya hawa vyura. Warekani kula vyara ni kama vile wanakula Kitimoto.


    Mdau Maryland- USA

    ReplyDelete
  6. VYURA WA Kihansi wanazaa ndo mana wa kipekee...

    ReplyDelete
  7. wana nchi tuna kufa njaa hali ngumu nyie mmekazania vyura !!! ebu ache masiara

    ReplyDelete
  8. Mdau wa juu anayeuliza vyura hawa wana faida gani ananishangaza sana. Kwani Mwenyezi Mungu alipowaumba na kuamua kuwaweka hapo Kihansi alitushauri? Labda nikuulize na wewe una faida gani hapa duniani?

    Mdau aliyeulizia ikiwa bado wapo Marekani hao vyura. Ni kwamba wako tena wengi tu. Serikali ilichukuwa hao vyura mia moja kwa majaribio lakini kule Marekani wako zaidi ya elfu sita.

    Vyura hao walikuwa wanafuatiliwa kwa makini huko Marekani na Serikali ya Tanzania. Na ijapokuwa hatuwezi kuthibitisha kwa asilimia mia moja kwamba wamebadilishwa au la, lakini imani yetu kubwa ni kwamba hawakubadilishwa kijenetiki.

    Huu ni urithi wetu watanzania kwani Mwenyezi Mungu alivyoamuwa kuwaweka pale Kihansi katika eneo lote la dunia hii alikuwa na maana yake ambayo siyo lazima tuielewe leo au kesho.

    Tayari kuna baadhi ya vyura ambao wameonesha kutoa kemikali fulani ambazo zinaweza kutumika kama dawa, inawezekana na hawa wa kwetu wakawa na faida kama hiyo baadae.

    ReplyDelete
  9. Tarehe Fri Sep 03, 10:13:00 PM, Mtoa Maoni

    hauna point wewe !!! blah blah blah una ngangania vitu visivyo na msingi , wakati wajanja wanachota madini tu


    wana nchi halingumu au vyura wachukulie wasichukulie awana faida zaidi ya sisi wana nchi

    ReplyDelete
  10. Hao chura wasije wakaanza kuzaliana kama senene wakawa wengi tukatakiwa kununua dawa za kuwapunguza kutoka huko kwao tena. Wasije wakaingia mtaani wakala mazao mpaka tukome..Imekuaje mpaka tumepewa hawa bila masharti????

    ReplyDelete
  11. kama america walikuwa wana wajali sana hao chura wange waacha huko kwao. wao wana pesa nyingi sana kwahiyo ingekua vizuri watumie pesa zao kuwatunza hao chura. sisi ni watu maskini watu wetu wana shida nyingi hatuna pesa za ziada kuwatunza hao chura. tusipo angalia hili kesho tutaambiwa kuna mijusi, panya na vijinyama vingine tuwatunze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...