Mratibu wa Jumuiko la Asasi za Kiraia Deus Kibabamba (katikati) akitoa tamko la uzinduzi wa mdahalo kwa wagombea uongozi wa nyadhifa mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa lengo la kutoa fursa kwa wananchi kuwahoji wagombea hao juu ya ahadi mbalimbali wanazozitoa watazitekelezaje badala ya kubaki kama wasikiliza wa hotuba za wagombea. Kulia ni Mjumbe wa Jumuiko hilo kutoka SHIVYAWATA Maria Chale na kushoto ni Mjumbe wa Jumuiko hilo Japhet Makongoro.


Na Tiganya Vincent, Dar es salaam

Jumuiko la Asasi za Kiraia limezindua mdahalo wa kuwakutanisha wagombea nafasi Uwakilishi, Ubunge na Urais hapa nchini ili kutoa fursa kwa wananchi kuwahojia juu ya ahadi mbalimbali wanazotia katika mikutano ya kampeni inayoendelea watazitekelezaje.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Jumuiko hilo Deus Kibamba wakati akisoma tamko la uzinduzi wa mdahalo huo kwa waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)

Alisema kuwa kampeni zinazoendelea hivi sasa wagombea wa vyama vyote vinavyowania nafasi ya kushika Dola wamekuwa wakihutibia tu bila kuwapa fursa wananchi ambao ndio wapiga kura fursa kuhojia au kuulizia juu ya ahadi ambazo wazitoa watazitekeleza endapo wataingia madarakani au kwani nini wanashindwa kuzitekeleza katika kipindi cha nyuma.

Kibamba alisema kuwa hatutaki wananchi wawe watu wa kupokea tu kila kinachoelezwa na mgombea na kuishia kupiga makofi bali pia washiriki katika kampeni kwa kuwahoji wagombea mbalimbali wa nafasi za Ubunge na uwakilishi.

Alisema kuwa kufuatia udhaifu katika undeshaji wa kampeni na ushirikishaji wananchi duni katika Kampeni Jumuiko la Asasi za Kiraia limeamua kuandaa mdahalo kwa ajili ya kuwapa fursa wagombea kunadi sera zao na kisha kuulizwa moja kwa moja na wananchi ana kwa ana au kutumia simu na baraua pepe.

Kibamba alitoa wito kwa wagombea wote kushiriki ili wapate fursa bure ya kueleza sera zao kupitia Redio na Televisheni kwa ajili ya kuwashiwishi wapiga kura ili wawape ridhaa ya kuongoza majimbo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema kuwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiko la Asasi za Kiraia utaendesheshwa katika majimbo zaidi ya mia moja na utakuwa sawa kwa wagombea toka vyama vyote vyenye wagombea katika majimbo.

Mdahalo huo utaanza kuonyeshwa moja kwa moja kutoka mkoani Ruvuma siku chache zijazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. safi sana. kazi nzuri anzeni mara moja. tunahitaji kuwahoji wagombea wote kwenye television na redio

    ReplyDelete
  2. chonde chonde uncle misupu,uwe unatuwekea full clips za hao wagombea wetu ilituweze kuchambua na kupambanua pumba zao.

    Pili,tafadhali sana mzee wa libeneke tupe details kamili,namaanisha email na namba zao za simu ili na sisi wabeba box tuweze kuchangia.

    ReplyDelete
  3. Huyo mdau anaitwa Japhet Makongo na si Makongoro kama mlivyoandika msije mkamsababishia matatizo yaliyompata Letitia 'Nyerere'. Tunasubiri sana midahalo maana tumechoka hotuba za kudanganyana kwa ahadi kibaoo! Ati mtu ukitaka kumwajiri akutumikie si ni lazima umfanyie usaili?!?! Wanasiasa acheni usanii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...