Wanafunzi wengi waliohitimu kidato cha sita na kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga na Vyuo Vikuu nchini Tanzania wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu sasa kupata majibu hayo, zoezi ambalo limechukua muda mrefu kuliko ilivyokadiriwa na hivyo kugeuka kuwa kero kubwa katika mipango ya watu, familia na wafadhili.

Linki ifuatayo ina orodha ya wale wote
waliochaguliwa na TCU kujiunga na chuo cha SAUT:
http://74.53.24.105/~saut/selectiontcu.php

Kwa bahati mbaya, tovuti ya Tanzania Commission for Universities, TCU, ambapo matokeo ya vyuo vyote yanatarajiwa kuorodheshwa, bado haina linki wala maelezo yoyote zaidi ya kusema matokeo yanatarajiwa kutoka tarehe za katikati ya mwezi Septemba na kuwa wanaomba samahani kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na zoezi hili.

Tafadhali endelea kubofya linki ya TCU kuona ikiwa wameshabandika matokeo: www.tcu.go.tz

Poleni sana kwa usumbufu mnaoupata,
ninaihisi shauku na hasira mliyo nayo. Poleni.

credit source:
http://www.wavuti.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Secondari za seminary zinafundisha na kufaulisha kwa kishindo kwa kuwa na misingi na rasilimali muhimu na imara.

    Hii haimaanishi kuwa vyo vikuu vya binafsi (seminary ukitaka) ni vizuri pia. Vyaweza kuwa vinajitahidi.

    Ni vizuri watu wapigane kwanza kupata vyuo vikomavu na vyenye walimu wakomavu wakutosha, wakikosa ndo waende kwengine.

    ReplyDelete
  2. TCU imedhirisha kutokuweza kutekeleza majukumu yake katika wakati hata ule ambao imejipangia wenyewe.mbaya zaidi imeshindwa hata kuomba radhi wanafunzi kwa kushindwa kwao kutekeleza jukumu lao kama walivoahidi kutoa selection tarehe 18september

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2011

    TCU waache siasa yao ya maji taka mambo ya Elimu hayahitaji
    siasa kwani wanachezea maisha ya vijana ambao ndio wajenga nchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...