Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, ( wapili kutoka kushoto) akisalimiana na mchezaji wa kiungo wa Yanga, Athumani Idd ( Chuji) wa pili kutoka kulia ,kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro. Timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Nsa Job ( kulia) akichuana na Beki mmoja wa timu ya Mtibwa karibu na eneo la hatari la Mtibwa , huku mlinda mlango Shaaban Kado akijiandaa kudhibiti hatari yoyote itakayojitokeza wakati wa mchezo wao uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini hapa, timu hizo zilifungana bao 1-1.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wadau, michezo tunaipenda ila kwa aina ya viwanja vyetu inakatisha tamaa. ona wachezaji wa kimataifa na taifa star wanavotimua vumbi utadhani ni mchezo wa enzi zenyewe najeza mpira wa vitambaa (daso) kule kijijini. Tuwekeze na kubadilisha mambo ili na sisi tufike mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...