Msemaji mkuu wa Supa Pesa Natasha Issa akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa milioni kumi Dr. Licky Abdallah


MSHINDI WA TATU WA MILIONI KUMI ZA SUPA PESA APATIKANA!

Mshindi wa tatu wa Milioni Kumi, Dr. Licky Abdallah mwenye umri wa miaka 52, wa bahati nasibu ya kipekee ya SUPA PESA amekabidhiwa hundi ya fedha hizo jana jijini Dar es salaam.

Dr. Licky Abdallah ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, ni mkurugenzi wa kampuni ya Malagarasi Tours and Safaris na pia ni mchambuzi maarufu wa wa mpira wa mguu (soka ) hapa jijini.

Alipokea hundi hiyo kwa furaha na kusema kwamba alikuwa akichukulia kama utani pale ambapo alisikia kuhusu droo hii ya Supa Pesa na kushiriki kama utani.


‘Ilitokea kama bahati kubwa pale ambapo nilipigiwa simu na kituo cha radio Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wangu. Kiukweli nilijawa na furaha sana. Pesa hizi nitaziongezea kwenye mtaji wa biashara yangu na pia kumtunuku zawadi binti yangu ambaye alinishawishi kushiriki droo hii ya Supa Pesa.’ Alisema Dr. Licky.

Msemaji wa Supa Pesa, Bi. Natasha Issa, kwenye zoezi la kumkabidhi mshindi huyo hundi yake,amesema kwamba washindi wanazidi kumiminika kila siku kutoka kila kona ya Tanzania.

Aliwataka watanzania wengi zaidi kushiriki droo hii ambapo kila siku kunapatikana washindi watatu wa milioni moja, na Mshindi mmoja wa Milioni Kumi kila wiki.


Bi. INatasha aliongezea kwa kusema,‘Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777.

Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA MR LEAKEY,ALIYENACHO ANAONGEZEWA,LAKINI KAKA HAPO OFISINI KWAKO MALAGARASI KUNA RUSHWA SANA BANA,HASA ABDALLA KAMA BADO YUPO JAMAA HATOI KAZI MPAKA UMPE KITU KIDOGO WAKATI KAZI YENYEWE NJAA TU,MWAMBIE AACHE KUBANA.

    ReplyDelete
  2. dr leakey mchawi bana,,kila kiiitu bingwa yeye tu...dah!me sikubali.

    ReplyDelete
  3. ...Marketing nzuri hiyo...

    ReplyDelete
  4. WIZI WA KISAYANSI,

    Shinda mkoko na vodacom, Zantel, tigo, zain. changia ccm, chadema, yatima nk na sasa huyu msanii mpya.

    ho tate nane!

    ReplyDelete
  5. Hongera dr likki; ijapokuwa wengi wetu tuna-prefer kukuona kwenye runinga ukichambua soka?

    ReplyDelete
  6. Siku hizi hatuhitaji wataalamu wa uchambuzi wa soka kama vile dk likky. Nakuomba ndugu michuzi blogu ya jamii ianzishe mchango ili tumnunue "pweza mtabiri" kama vile pweza paul atutabirie matokeo ya mechi na biashara itakuwa imekwisha. mimi sili pweza lakini ni mshabiki wa pweza paul.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...