Mgombea Ubunge kwa chama cha CHADEMA,Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akiwahutubia wakazi wa Kata ya Nyamatare Musoma mjini jana ikiwa ni sehemu yake ya kuwanadi wagombea wa chama chake,hapa alikuwa ndani ya jimbo la Musoma Mjini ambapo Vincent Nyerere anagombea jimbo hilo.
Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,Bw.Vincent Nyerere akijinadi kwa wananchi jana jioni Katika Kata ya Nyamatare,jimbo la Musoma Mjini.
Mgombea Ubunge kwa chama cha CHADEMA,Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akimnadi Mgombea Ubunge katika Kata ya Nyamatare jimbo la Musoma Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,Bw.Vincent Nyerere akijinadi kwa wananchi jana jioni.kwa picha zaidi bofya hiyo link hapo chini.
http://zittokabwe.wordpress.com/


SISIMU presha inapanda presha inashuka. Hongera Zitto tunataka mabadiliko. SHinyanga mjini lini kuongeza nguvu?
ReplyDeleteMdau mpenda mabadiliko ya kweli
Zitto vaa magwanda acha ubishoo. Samahani Mheshimiwa ila CHADEMA tuna sare. Ni hayo magwanda ya khaki.
ReplyDeleteHongera CHA-DE-MA cham la wazawa.
ReplyDeleteKigoma kaskazini
Arusha
Ubungo
Musoma
Mbeya
Tunaelekea Dodoma kwenye mjengo kutetea haki.
huyu Vincent Nyerere sijamsikia katika orodha ya watoto wa kambarage, hebu nitaarifuni! ni mtoto wa nje ya ndoa au ameokota jina ili apate ubunge kirahisi?
ReplyDeleteAnon wa kwanza, CCM hatuna pressure kabisa; pressure iko chadema kwa sababu huo ukali wenu chadema ni ukali wa soda na ndiyo maana mbio zenu zitaishia ukutani 31/10/2010. ccm4life.
ReplyDeleteKwa taarifa tu Vincent si mtoto wa Mwalimu; watoto wa Baba wa Taifa wako katika kampeni ya CCM: hasa Makongoro, Madaraka na Rosemary. Machegeson.
ReplyDeleteHongera sana mh. Kabwe, wewe ni mwanamapinduzi wakweli, wewe ni mfano wa kuigwa na vijana wote wa tanzania. mwanza unakuja lini kuongeza nguvu kwa Mh. Wenje? tunakusubiri uje kuongeza chachu ya ushindi wa kishindo jimbo la nyamagana.
ReplyDeleteMimi kijana mwenzako mpenda mabadiliko.
Msangi.
Zedi si uje A town tunakuzimii sana
ReplyDeleteArusha ni wachaga tu ndio wako chadema, wengine wooooteeee tuko CCM.
ReplyDeleteVincent Nyerere ni mtoto wa Josephat Kiboko, mdogo wa Julius Nyerere!
ReplyDelete