Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo katika kijiji cha Kibeni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kiongozi wa Wanachama 70 wa Chama cha Wananchi CUF Jimbo la Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja Ali Suwedi, akimkabidhi Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein Jumla ya kadi 70 za CUF kwenye mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo katika kijiji cha Kibeni Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya Wanachama hao kuamuwa kukihama Chama hicho.
Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakimskiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliopfanyika leo katika kijiji cha kibeni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
umati mkubwa wa wana CCM wa kijiji cha Kibeni mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM,Dr. Ali Mohamed Shein leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Asante Michuzi kwa picha za mgombea urais kupitia CCM zanzibar lakini hiyo picha ya pili ni watu waliofikishwa hapo kuengeza idadi kwani mimi kwetu ni kibeni baba na mama bibi yangu mzalia mama wazazi wake wametokea Mkwajuni na ukoo wetu umarufu ni kwa shekhkinyamoto mumgu amrahamu hakuna watu wenye tamaduni kama hiyo kibeni hilo wazee wa hapo hawalikubali hata siku moja lifanyike kwa mwanamke anaetokana na chimbuko la hapo hapa sisemi kwa ubaguzi lakini hata sura zinakupa picha halisi

    ReplyDelete
  2. Mkuu Michuzi.
    nakuona unavyojenga na kupromoti DEMOKRASIA kwa kuamua kuhabarisha umma upande mmoja wa shilingi.
    Tusiogope changamoto tuwe mstari wa mbele kuonesha non bias.

    ReplyDelete
  3. kaka michuzi tumechoka na chama kimoja try to be fair

    ReplyDelete
  4. MONOPATIZM ATITUDES.
    KABLOG KA SISIEM.
    KUWA FEA KWA VYAMA VINGINE.

    ReplyDelete
  5. SASA NDIO NIFAHAMU KWA NINI YANGA WAKIPIGANA BAKORA WANAENDA ZENJI KUANGUKIA CCM NI CHAMA CHA WAZALENDO AKA WANZANZIBARA NA WAPINZANI WENGI NGOZI ZA KUPINDUA NA NDIO SIMBA YANGA OYEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  6. KAKA MICHU AMEKUWA AKIZUNGUKA NA TIMU YA CCM HIVYO NI RAHISI KUPATA HABARI NA KUZIPOST. ALIWAHI KUANDIKA WAKUSANYAJI WENGINE WA HABARI ZA VYAMA VINGINE WAZILETE NA AMEPOSTI MARA KIBAO, AU MNAOLALAMIKA NI WAGENI KTK HII BLOG? KARIBUNI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...