MAREHEMU DEVOTA SIMPERT KINUNDA

Familia ya Marehemu Dr Simpert Kinunda wa Ubungo Msewe, wanapenda kutoa shukurani zao za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi katika Kuuguza na hatimaye Kifo cha Mama yetu Mpendwa Devota S Kinunda kilichotokea tarehe 16/8/2010, sio rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja tunaomba mpokee shukurani zetu za dhati,

Ni miezi miwili sasa tangu Mama yetu mpenzi ututoke. Sisi wanao (Rosalinde Kinunda Mussa, Nicodemus Kinunda, Donatha Kinunda na Omega Kinunda) Bila kusahau wakwe na wajukuu zako Tunakukumbuka kwa uvumilivu wako, hekima, upendo na ushauri.

Familia ya marehemu Dr. Simpert Kinunda inawakaribisha kwenye misa ya shukurani ya kumwombea marehemu Mama yetu, tarehe 16 October 2010 katika Parokia ya Ubungo Msewe saa 12 na nusu asubuhi na katika sadaka itayafanyika nyumbani kwa marehemu Ubungo Msewe [Golan] kuanzia saa 6:00 mchana

Karibuni wote

Mama tulikupenda ila Baba amekupenda zaidi

Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni sana Roseline, Musa and the family.

    Clemens

    ReplyDelete
  2. Poleni sana: Mama huyu alikuwa mwalimu na Mlezi shupavu, mwenye Imani Pevu ya Ukikristu; Alitusaidia sote wanajumuiya ya Muhimbili hususani JKM (Jumuiya Katoliki Muhimbili). Mungu amlaze mahali pema, na fadhili zake hapa dunia ziwe masurufu yake huko Mbinguni: Basi wanafamilia tunoamba mmojawapo atupatie njia ya wasiliano ya simu tuweze kutoa pole.

    Fr. Ngirwa, A

    ReplyDelete
  3. oooohhh Pole sana Jibu na kaka Musa jamani....Doreen

    ReplyDelete
  4. Poleni sana, Mungu wa upendo na awape nguvu.

    Kunda

    ReplyDelete
  5. Ooohhh Mungu wangu jamani Mwl. Kinunda wetu jamani. Bila Mwl. Kinunda wengine tusingefika hapa tulipo, she was a teacher, mother and friend. Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi. Michuzi tunakushukuru sana kwa kutujulisha Msiba huu kwani umetugusa tulio weng na tulio mbali na nyumbani ambao kwa kweli tungetaka kumzika mama na mwl wetu mpendwa.
    Mungu awatangulie na awape nguvu watoto na wajukuu wote wa mwl. Kinunda na tutamkumbuka daima.Ameni.
    Joy.

    ReplyDelete
  6. wanasema hakuna zaidi ya mama,nilikuwa nachukujia juu juu tu huu msemo,lakini ni kweli usio na uongo.ilikuwa ni ngumu kuamini kama siku moja mama atakuja kutoweka na tusimwone tena.mama umekuwa kwangu mwanga ambao ulikuwa ukiniangazia,ingawa umeenda lakini nuru ya mwanga wako bado niyo moyoni.nakupenda sana mama.pumzika kwa amani.ur son omega

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...