Katibu Mkuu wa Chama cha Wasioona Tanzania Bw. Emanuel Saimon akichapa risala ya chama chake katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga bi. Amina Masenza akiangalia fundi cherehani ambaye ni mlemavu asiyeona Bw. Abdallah toka wilaya ya Temeke akikata nguo.
Fundi simu ambaye ni mlemavu asiyeoona toka wilaya ya Temeke akitengeneza simu katika maadhimisho hayo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. MAajabu ya mungu ni makubwa sana.

    Mdau paris

    ReplyDelete
  2. Hii ni changamoto sana kwa watu wote...

    ReplyDelete
  3. Umenikumbusha Ami yangu Maalim Kali, Mwenyeezi Mungu amrehemu, Amin.
    Yeye alikuwa mlemavu asiyeona lakini alikuwa anafanya kazi zake vizuri na alikuwa fundi mzuri wa redio.
    Ni Kweli maisha bila kuona yanawezekana!

    ReplyDelete
  4. Michu,
    Typo zimezidi. Tafuta editor.

    ReplyDelete
  5. Ingebidi wanaume ndio wapewe kutokuona ili wapunguze kucheat

    ReplyDelete
  6. Astaghafirulahi. We anony wa 02:38:00 Unamwogopa Mungu kweli? Umechanganyikiwa au frustrations???
    Hata wewe kuna unaowakosea, unajua laana ngapi wamezitoa kwako na ingekuwa hivyo kila mwanaadam unachomwombea mwenzio anakipata leo hii kwa choyo za kibinadamu si ingekuwa balaa duniani?
    Tena unafikiri mtu asipoona ndio hawezi kuwa na tamaa kama ni tabia yake??
    Muombe mwenyezi Mungu akusamehe kwa hilo ulilolitamka. Unafahamu msemo usemao maneno yanaumba? Na unafahamu kuna imani kwamba unapotoa neno baya linazunguka duniani ili kumfikia aliyelengwa na likimkosa linarudi lilipotoka??

    Ehh mwenyezi Mungu tupe moyo wa uvumilivu. Amina.

    Mama Fatu.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Walemavu nao wanaweza. Binafsi nimepata bahati ya Kufundishwa na Mlemavu huyo mnayemwona hapo juu Mwl.Simon ni mwalimu mzuri sana wa History One ya A-level. Alikuwa anatufundisha vizuri sana na somo lake tukiaulu sana pale Mkwawa High School enzi hizo. Kwa kweli serikali na jamii nzima tunatakiwa kuwaangalia kwa jicho la ukaribu,kuwasaidia na kuwawezesha hasa kielimu na mtaji

    ReplyDelete
  8. Ingebidi wanaume ndio wapewe kutokuona ili wapunguze kucheat
    _____________________________________

    Nilicheka na hii point yako ila najua unakotokea, katika usichana wangu nilitapeliwa sana na wanaume mpaka niliomba ingekuwa hivyo ila namshukuru mungu kanipa mume ambae katulizana na kuridhika na mie kwa jinsi nilivyo.

    point yangu ni kwamba kama hakufai achana nae endelea kutafuta mwingine, usikae tu ukaomba mabaya shugulika upate wako.

    stay blessed my dear

    ReplyDelete
  9. duh lakiniutafikiri wanaona kwa mbali walivoziinamia hizo type na computer! By the way hy alosema wanaume wapofuliwe hiyo sio dawa kwa kuwa HATA GIZANI MTU HAKOSEI ANAPELEKA NDIPO KISU KWENYE ALA USHIKE ADABU YAKO TENA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...