Pia Mh. Taj aliwaasa Watanzania waishio Ufaransa wawe mabalozi wazuri wa Tanzania. Aliwaasa kutangaza sifa nzuri na fursa zilizopo kama vile uwekezaji, utalii na mengineyo mazuri ili kuitangaza nchi kwa uwepo wao na katika shughuli zao wawapo ugenini.
Akigusia Uchaguzi Mkuu, Mheshimiwa balozi alisema kuwa Tanzanaia bado ni nchi changa kisiasa na kidemokrasia hivyo si rahisi kwa watanzania walio nje ya nchi kushiriki katika kupiga kura kwa sasa.
Mheshimiwa Taj aliwapongeza pia Watanzania waishio Ufaransa kwa kuunda Chama cha Watanzania Ufaransa (CCWU) kinacholenga kuwaleta pamoja Watanzania. Chama hicho cha Watanzania kiliundwa mwaka 2007. Baadhiy ya malengo ya CCWU ni kutangaza na kukuza utamaduni wa Kitanzania nchini Ufaransa, kuendeleza ufundishaji wa lugha ya Kiswahili; na pia kutangaza utamaduni wa kitanzania kupitia matamasha na shughuli nyingine za kitamaduni. Pia CCWU huunganisha Watanzania waishio Ufaransa katika raha na majonzi.
Kwa sasa viongozi wa CCWU ni Delly Makombe (Mwenyekiti), Elizaphan Manda (Mwenyekiti msaidizi), Pamella Assey Lombard (Katibu) na nafasi ya Mweka Hazina inashikiliwa na Kemilembe Kazaura Monot.
Hizi habari weka week ijayo maana zinatujazia tu nafasi sisi tunahitaji matokeo tu saa hizi. Nothing more or less!
ReplyDeleteN.America
Not now..Tulivyokua tunakuja kutafuta habari ulikua kila siku unaweka makampain picture huku. Leo ninarefresh kutafuta mambo ya uchaguzi unaweka habari nyingine...Leo weka siasa tu...tuko huku tunafungua blog yako kila dakika 10 kwa ajili ya uchaguzi....Please please please kaka Michu okay...thanks
ReplyDeleteWe anon wa kwanza unayejiita eti N. America, wacha udikteta wako wa kishamba!!!! Speak for yourself, usitake kutuburuza!!!!damn it!!!!!
ReplyDeleteS America.
Hiyo idara ya diaspora isiwe blah blah. Rwanda wamewezeshwa kupiga kura kutipitia ofisi zao za ubalozi. Tanzania imeshindwa nini? au ndo yale yale ya kuogopa wasomi na walio nje kwakuwa hawadanganyiki??
ReplyDeleteWatuambie kama ni gharama tulipe $50 kujiandikisha kupiga kura tupo tayari. Waache uzushi!!
You must be kidding. Walionje wengi ni anti establishment. Kweni serikali inawazimu?
ReplyDelete