Mh. Balozi Begum Karim Taj, Balozi wa Tanzania Ufaransa. Chini akiwa na baadhi ya Watanzania waishio Ufaransa alipokutana nao
Katika mkutano huo na Watanzania waishio hapa Ufaransa, Mh Taj alisisitiza kwamba serikali ya Tanzania ina thamini sana raia wake waishio nje ya mipaka ya Tanzania. Alifafanua kwamba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanzisha idara maalumu itayoshughulikia masuala ya watanzania waishio nje ya Tazania (diaspora) ili kujua mahitaji yao, idadi yao na uwezo wao hususani kielimu na kifedha ili kuona ni namna gani wanaweza kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Pia Mh. Taj aliwaasa Watanzania waishio Ufaransa wawe mabalozi wazuri wa Tanzania. Aliwaasa kutangaza sifa nzuri na fursa zilizopo kama vile uwekezaji, utalii na mengineyo mazuri ili kuitangaza nchi kwa uwepo wao na katika shughuli zao wawapo ugenini.

Akigusia Uchaguzi Mkuu, Mheshimiwa balozi alisema kuwa Tanzanaia bado ni nchi changa kisiasa na kidemokrasia hivyo si rahisi kwa watanzania walio nje ya nchi kushiriki katika kupiga kura kwa sasa.

Mheshimiwa Taj aliwapongeza pia Watanzania waishio Ufaransa kwa kuunda Chama cha Watanzania Ufaransa (CCWU) kinacholenga kuwaleta pamoja Watanzania. Chama hicho cha Watanzania kiliundwa mwaka 2007. Baadhiy ya malengo ya CCWU ni kutangaza na kukuza utamaduni wa Kitanzania nchini Ufaransa, kuendeleza ufundishaji wa lugha ya Kiswahili; na pia kutangaza utamaduni wa kitanzania kupitia matamasha na shughuli nyingine za kitamaduni. Pia CCWU huunganisha Watanzania waishio Ufaransa katika raha na majonzi.

Kwa sasa viongozi wa CCWU ni Delly Makombe (Mwenyekiti), Elizaphan Manda (Mwenyekiti msaidizi), Pamella Assey Lombard (Katibu) na nafasi ya Mweka Hazina inashikiliwa na Kemilembe Kazaura Monot.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hizi habari weka week ijayo maana zinatujazia tu nafasi sisi tunahitaji matokeo tu saa hizi. Nothing more or less!

    N.America

    ReplyDelete
  2. Not now..Tulivyokua tunakuja kutafuta habari ulikua kila siku unaweka makampain picture huku. Leo ninarefresh kutafuta mambo ya uchaguzi unaweka habari nyingine...Leo weka siasa tu...tuko huku tunafungua blog yako kila dakika 10 kwa ajili ya uchaguzi....Please please please kaka Michu okay...thanks

    ReplyDelete
  3. We anon wa kwanza unayejiita eti N. America, wacha udikteta wako wa kishamba!!!! Speak for yourself, usitake kutuburuza!!!!damn it!!!!!
    S America.

    ReplyDelete
  4. Hiyo idara ya diaspora isiwe blah blah. Rwanda wamewezeshwa kupiga kura kutipitia ofisi zao za ubalozi. Tanzania imeshindwa nini? au ndo yale yale ya kuogopa wasomi na walio nje kwakuwa hawadanganyiki??

    Watuambie kama ni gharama tulipe $50 kujiandikisha kupiga kura tupo tayari. Waache uzushi!!

    ReplyDelete
  5. You must be kidding. Walionje wengi ni anti establishment. Kweni serikali inawazimu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...