BENDI ya K-Mondo Sound sasa imeamua kufanya mashambulizi ya kujitangaza baada ya kuamua kuachia nyimbo mbili kwa mpigo mmoja ukienda kwenye redio na mwingine kwenye televisheni.

Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino alisema mjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa baada ya kutengeneza video za Njiwa na Your Still Mine waliona watangulize wimbo mmoja kwenye redio huku mwingine ukipelekwa kwenye redio.

“Tangu Mhina (Panduka) ajiunge na bendi yetu, wimbo wake wa kwanza kutunga akiwa na K-Mondo sasa tukaona tuupeleke redioni ili watu wamsikie mkongwe huyu akiwa anatambaa na mduara,” alisema.

Kuhusu video, alisema wamepeleka kwanza Njiwa kutokana na kuiangalia Your Still Mine na kuona inatakiwa kuongezewa vitu vingine.

“Njiwa kwa mara ya kwanza tuliitambulisha kwenye mtandao wa FaceBook, tulipata maoni mbalimbali ambayo yakatupa moyo na tukaamua kuipeleka moja kwa moja kwa Televisheni,” alisema.

Mangustino alisema wamejipanga vizuri kwa ajili ya uzinduzi wao ambao utafanyika mapema mwakani. Alisema kwa sasa bendi yao inafanya maonyesho yake kila Ijumaa katika ukumbi wa Triz Motel uliopo Mbezi wakati Jumamosi wanahamia City Hotel pia Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...