Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma leo mchana.Kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu SMZ Dk. Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu CCM Yusuf Makamba, Makamu wa CCM Bara, Mh. Pius Msekwa na Rais wa Zanzibar Dk. .Ali Mohamed Shein.
Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano aliyemaliza muda wake Samuel Sitta akimpongeza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kwa kuchaguliwa tena kuendelea na wadhifa huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma
Spika aliyemaliza muda wake Samuel Sitta akisalimiana na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Hongera 6, umeliongoza Bunge lililopita kwa kasi na viwango.Historia haitakusahau
ReplyDeleteurafiki wa mashaka
ReplyDelete