Rafiki mtafutwa, Lucas Alfred

Hallow Ankal Michuzi pamoja na timu yako nzima ya blog ya jamii ,kwanza naomba nikupe pole sana kwa kazi hii ngumu na mhimu sana,kwani siye wadau tuliyo nje ya nchi tunajivunia sana uwepo wa blog hii na pia inatusaidia sana ktk kupata habari kwa haraka sana kutoka nyumbani pia dunia nzima kwa ujumla.

Leo Ankal naomba sana unisaidie kumtafuta huyu rafiki yangu ambaye nimepoteza nae toka mwaka 2001 na kwa mara ya mwisho tulionana jijini Dar nyumbani kwa mama yake aliyekuwa anaishi kwenye nyumba za polisi.Jijna lake ni LUCAS ALFRED na mama yake alikuwa ni askali (trafik) pia kwa tetesi nilizo nazo ni kwamba hata yeye alikwenda ktk fani hiyo ya uaskali japo sina hakika na hilo.Nimesoma nae Shule ya secondary Sangu jijini mbeya kati ya 1997-1998 na baada ya hapo alihamia jijini dar ambapo ndipo alipo malizia elimu yake ya secondary katika shule ya secondary ya jitegemee.

Mimi kwasasan ipo nchini uingereza na jina langu la utotoni ambalo huenda hata yeye atalitambua rahisi zaidi BARAKA EDWARD, Kwa atakaye kuwa na taarifa zake basi awasiliane na mimi kwa simu namba
+447725694894
au barua pepe
raymonds19@yahoo.com
Natanguliza shukrani zangu kwako.
Ndimi mdau Baraka Edward

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mi namfahamu huyu bwana anayetafutwa kama mama yake alikuwa ni askari na sio askali. Na ninavyofahamu ni kuwa naye sasa ni askari, lakini kama unaongelea jamaa ambaye ni askali basi simjui. Nawakilisha

    ReplyDelete
  2. You are such a good friend and a good person and may the Lord Bless you more, waswahili walisema RAFIKI MZURI AWEZA KUZIDI NDUGU MBAYA, HII INAMAANA RAFIKI YAKO WA KWELI AWEZA KUWA NDUGU YAKO. So ho[e huyu mtu atapata msg yako and he will get back to you and keep your relationship and your friendship SHINE MORE AND MORE. Stay Blessed.

    ReplyDelete
  3. Nashukuru sana wadau kwa msaada wenu na moyo wa kujituma kusaidia.Yule rafiki yangu niliyekuwa namtafuta amepatikana na hivi sasa nina mawasilano nae baada ya mda mrefu kupita asanteni sana wadau.Na pia nashukuru sana mdau wa lugha nimekupata japo nadhani yule uliyekuwa unamfahamu hakuwa yeye....ila shukrani sana kwa mchango wako.

    ReplyDelete
  4. Mimi FUraha Laizer wa Arusha Namtafuta Rafiki yangu tumepoteana naye Miaka mitano sasa na sina mawasiliano nae nilikuwa nina namba zake ila sasa hivi hazipatikani tulisoma nae Arusha Tropical Center, na alipata Kazi AIR TANZANIA ILA KWA SASA SIJAJUA KAMA YUPO HAPO AU HAYUPO NAOMBA MNISAIDIE MKPATA ASANTE EMAL YANGU NI furahacharles@hotmail.com

    asanten

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...