Na Dixon Busagaga
KLABU ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro(MECKI) ambayo ilikumbwa na migogoro kwa muda mrefu imepata viongozi wapya watakaoiongoza kwa muda wa miaka mitatu ijayo.

Katika uchaguzi huo uliotawaliwa na kampeni kali kama zilivyo kwenye vyama vya siasa,baadhi ya wakongwe akiwamo mwenyekiti wa muda wa klabu hiyo,Josephine Sanga walibwagwa.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Arusha,Claud Gwandu kwa kushirikiana na katibu msaidizi wa chama cha waandishi wa habari wa Manyara,Yusuph Dai.

Akitangaza matokeo hayo,Gwandu alimtaja Mratibu wa radio Boma Hai Fm inayomilikiwa na halmashauri ya Wilaya ya Hai,Hilda Kileo kuwa mshindi baada ya kumwangusha aliyekuwa mwenyekiti wa muda,Josephine Sanga kwa kura 21 dhidi ya 16.

Katika ya makamu mwenyekiti,mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo,Rodrick Makundi alishinda kwa kura 25 huku mpinzani wake Nakajumo James wa HABARILEO akipata kura 14.

Nafasi ya katibu mkuu mtendaji imechukuliwa na mtangazaji wa radio Moshi Fm,Yusuph Mazimu ambaye alishinda kwa kura 30 dhidi ya kura 11 za mpinzani wake Salome Kitomary wa Nipashe..

Nafasi ya katibu msaidizi Nakajumo James aliibuka na ushindi mdogo wa kura 21 huku mpinzani wake wa karibu Samwel Shao wa Jamboleo akipata kura 20.

Nafasi ya mweka hazina alichaguliwa Jane Mhalila kutoka chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara cha Moshi(MUCCoBS) kwa kura 30 huku mpinzani wake,Rehema Matowo akipata kura 11.

Wajumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Salome Kitomary(Niapshe)Suzan Ngeiyamu,(Sauti ya injili)Bahati Mustafa(Moshi fm), Jackson Kimambo(Niapshe),Dixon Busagaga(Moshi fm/Tz daima) na Hellen Madege(Sauti ya Injili).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kama viongozi ndo hao, sitegemei maendeleo yoyote ya club hiyo. Wanaobisha wasubiri mwaka ukatike kama watakuwa wameona mabadiliko yoyote wanipige faini. Yetu macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...