(24th May 1948 -- --29th Nov.1996)
Leo tarehe 29,Mama yetu mpendwa umetimiza miaka kumi na nne (14yrs) kamili tangu kufariki kwako.
Pengo uliloliacha ni kubwa mno kwani hakuna wa kuliziba!! Upendo na mafundisho yako daima tunavikumba sana.
Kwa sababu hatuwezi kupingana na mipango ya MUNGU na pia naamini MUNGU alikupenda zaidi ya sie tulivyokupenda ndio maana alikuchukuwa!!! Unakumbukwa sana na mwanao wa pekee Ruth,mkweo Eugene na wajukuu zako Emily na Ervin.
Pia unakumbukwa sana na watoto wako, dada zako, kaka zako,wadogo zako,wifi na shemiji zako,ndugu, jamaa na marafiki.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!!!
Ruth (Mama Emily na Ervin)
ReplyDeleteMimi na Mke wangu Doris Mwanza pamoja na familia yote tunajiunga nawe katika kuikumbuka siku hii ya pekee aliyotutoka mama yetu mpendwa. Tunamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa maisha aliyotupatia sisi sote na Mama Mpendwa. Tuendelee kumtegemea yeye katika yote. Amin
Wasalaam, Shemeji yako Urio (Botswana)
R.I.P Mama mdogo, daima tutakuenzi kwa kutenda yale mema uliyokuwa ukituelekeza, tunakosa busara na upendo wako kwa kiasi kikubwa, kimwili haupo nasi lakini kiroho upo pamoja nasi. Jina la Bwana lihimidiwe. Amen
ReplyDeleteMazila