Kutokana na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa jijini dar,umepelekea taa nyingi ya kuongozea magari barabarani kutofanya kazi kutokana na mgao huo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizi kama ionekanavyo picha hii.hapa ni katika mataa ya Kinondoni studio,jioni ya leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. hivi hiziz taa za barabarani haziwezi kufanywa ziwe zinatumia solar wakati umeme ukikatika na wakati wa mchana?

    ReplyDelete
  2. CCM, CCM, CCM, CCM

    ReplyDelete
  3. hii nchi utafikiri haina mwenyewe, mungu ibariki tanzania lakini usiwabariki watu wake.

    ReplyDelete
  4. wakati hizi zina fanya kazi utaona
    matarafiki wana uongoza.wakati zikizima na hava matarafiki wana potea

    ReplyDelete
  5. Mdau hapo juu taa za solar mbona zipo siku nyingi bongo. Ila tatizo kasi ya kuzisambaza katika makutano mbali mbali ya barabara ni ndogo. Mfano mzuri ni mataa ya TAZARA ambayo yanatumia nguvu za jua. Yanafanya kazi kwa ufanisi mpaka raha yani.

    ReplyDelete
  6. kama hawaezi kazi basi watangaze watu wajitoleee kuweka solar power ili taa zifanye kazi.

    wao hawajali yote si wanasafishiwa barabara. wanapita udhaani wamebakia wao kwenye dunia hii.

    ReplyDelete
  7. waliokuwa madarakani kazi kuweka hela mifukoni na kuchoma kiti moto na makalio yao..hamna cha maana wanachokifanya..pumbaf..! Mungu nibariki nisirudi Tanzania.. Shenzi typ.......!

    ReplyDelete
  8. Taa za traffic za solar zipo -- naconfirm kwa mtoa maoni wa kwanza. Nimeziona sehemu kadhaa hapa Marekani (Texas) -- zinatumika wakati barabara zianjengwa hasa kwenye intersection. Nilinote jina la kampuni kwenye mabango niliyonaona --- http://www.horizonsignal.com/ ---. Goodluck kumwelewesha mhusika yeyote Dar kwamba taa za solar ndo zinafaa hapo kwetu

    ReplyDelete
  9. Cha ajabu, utakuta taa za barabara na hata saa za mitaani huwa zinatumia nyuzi za jua katika sehemu nyingi duniani. Taa kama hizi pia ni rahisi na hazihitaji matengenezo makubwa. India, China na Brazil wanatengeneza na kutumia na ni rahisi. Sisi tuna wasomi wa kila aina lakini hatujaaliwa na akili ya kujiendeleza, tunasubiri kupewa bure. Hata siku moja sijaamka na kujuta kuondoka Tanzania.

    ReplyDelete
  10. Huu ujinga kweli. Vekesheni yangu imeshaharibika. Inabidi nipunguze siku sasa ya kukaa Tanzania. Inaudhi kweli. Tunapata wiki mbili kupumzika nyumbani Krismasi na wanataka tukae katika giza halafu wanatumia fedha nje kuwaalika watalii waje kutembea katika giza. Mtakaa wenyewe huko.

    ReplyDelete
  11. Hivi ze gavamenti inajua watu wangapi wanaishia kukwanguana na magari yao kwasababu tu kisa Tanesco? ajali kubwa barabarani na mahospitalini watu kukosa umeme.

    acha viwanda!

    halafu fununu nikuwa hawa jamaa zake uncle michuzi nasikia wamekalia rasilimali umeme kule mtwara, umeme wa miaka kede ijayo? michuzi washauri basi siyo kuwapiga picha tu, halafu ubane na hii coment kama kawaida yako

    pyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  12. Huu ujinga kweli. Vekesheni yangu imeshaharibika. Inabidi nipunguze siku sasa ya kukaa Tanzania. Inaudhi kweli. Tunapata wiki mbili kupumzika nyumbani Krismasi na wanataka tukae katika giza halafu wanatumia fedha nje kuwaalika watalii waje kutembea katika giza. Mtakaa wenyewe huko.

    Fri Nov 26, 08:39:00 AM

    WEWE KWENU NI KWENU TU, NJOO MBONA MAMILIONI YA WATANZANIA TUPO NA MGAO WETU WA UMEME NA TUNAISHI. NJOO UONGEZE NGUVU YA KUIBOMOA TANESCO

    ReplyDelete
  13. Michuzi inaeleweka wewe ni mpambe wa CCM, nimetoa maoni ya kuichambua serikali na JK kuhusu uzembe unaoendelezwa msimu huu wa pili, umebania.

    Hata ukibana tunazo sehemu nyingi za kutoa maoni yetu, ukweli ni kwamba walimpa JK kura zao, sasa wanapata mavuno yao, hata mwezi aujapita Tanesco wanaendeleza uzembe wa msimu uliopita.

    Tumechoshwa na uzembe TZ, serikali itoke madarakani kama imeshindwa kazi, umeme karne nzima ni ttz, wanachoshangaa ni nini.

    Vyama vipo vingi vyenye sera nzr na nguvu mpya ya kuondoa mttz, vipewe nafasi.

    Tz imeoza

    ReplyDelete
  14. aaah mdau hapo juu umekosea, sema Mungu ibariki tanzania na watu wake usiwabariki viongozi wake!!

    ReplyDelete
  15. HE HE HEEEE SIPAMISI BONGO HATA DAKIKA MOJA...... AHERA HAKUENDEKI, BONGO HAIKALIKI NIMEPATWA NA MFADHAIKOOOOOOOOOOO......

    ReplyDelete
  16. Ajabu ni kwamba Traffic kukiwa na umeme nao wamo barabarani kuongoza magari...kama hakuna umeme nao wanakaa pembeni mwa barabara kungojea ajali...kweli Nahodha utaweza! Saidi Mwema taasisi hii ni ya taaluma si siasa...tuache kufanyakazi kwa maslahi ya tumbo tuuu. Nyerere baba ukisema utatuombea... Tuombee sasaaa Taifa lako linaenda ndivyo sivyo...naipenda Tanzania.. Bite

    ReplyDelete
  17. mkome kusapoti uchakachuaji. mkome na mgao wenu. niu mavuno ya uchakachuaji hayo. ni kweli kuwa sisyemu imetenda mambo mengi makubwa ambayo si rahisi kuyasahau, hili la ume me likiwa mojawapo.
    wapinzani hamna sera, mna njaa kali tu, na uchu wa madaraka uliokithiri, mnataka kwenda i ku ru kufanya nini? pale si mahali pa mchezo.
    Mnataka tenesko wawape umeme kila taim na kwa watu wote, kwani tutajuaje tofauti kati yetu? vingunge razima wajulikane bwana.

    halafu, kwani hamjuhi kuwa mvua haikunyesha kule kwenye bwawa la jimbo la mzee ciguiyemici? Alah, hamna adabu nyie! ngojeni mwaka 2015 kishindo kingine!

    ReplyDelete
  18. Hongera tumechaguwa maendeleo.

    ReplyDelete
  19. jamani! jamani! jamani! jamani,mi kama mtanzania sijui nifiche wapi sura,ni aibu,tunaonekana kama ming'ombe kwa jinsi viongozi wasivyo na mpangilio.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...