Mchezaji wa zamani wa Timu ya Yanga , Said Mrisho ‘ Zicco wa Kilosa’ aambaye kwa sasa ni mwalimu wa soka , akipata ushauri kutoka kwa Ofisa Lishe wa mpango wa huduma na tiba na Virusi vya ukimwi kwa lugha ya kingereza ‘ Management and Development for Health ( MDH) , aliyejitambulisha kwa jina moja la Charry , kwenye banda hilo na kumjulisha mchezaji huyo kuwa lishe yake ni nzuri licha ya kuwa hana maambukizi ya VVU. Lugha ya alama kwa walemavu wa kutosikia ‘ viziwi’ nayo ilitawala kwenye mabaanda ya maonesho ya wiki ya kilele cha siku ya Ukimwi Duniani , ambayo Kitaifa inafanyika Desemba Mosi, mwaka huu , Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Mipango wa Shirika la Maendeleo ya Watu nchini , ( HDT) ,Malanilo, Simon ( kushoto) akiwa pamoja na Mwandishi Mkongwe nchini na Mkufunzi mshauri , George Nyembela , wa AJAAT , wakitoa maelezo juu ya kampeni ya kupunguza maabukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto walipokutana na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani ) Novemba 30, mwaka huu, ikiwa ni siku ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi, mwaka huu, kitaifa yanafanyika Mkoani Morogoro.
Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Morogoro , SUA, MZUMBE na Chuo Kikuu cha Waislamu wanaunda shirikisho la CCM la Vyuo Vikuu, wakisoma taarifa ya kumpongeza Rais Dk Jakaya Kikwete, kwa kuchanguliwa kuongoza nchi , pamoja na uteuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda sambamba na Mawaziri wachapakazi.
Picha zote na John Nditi wa
Globu ya Jamii Mji kasoro bahari





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Utu unataka kumshinda ustaadhi picha ya tatu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...