Na Prosper Minja.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya ya Muungano wa Tanazania Mhe. Anne Makinda ameondoka nchini leo kwenda Namibia kuhudhuria mkutano wa jukwaa la mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC-PF.
Spika Makinda amepitia nchini Afrika Kusini na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe.Radhia Msuya ambaye pamoja na mambo mengine walipata wasaa wa kuzungumzia masuala ya nyumbani, uchumi na siasa kwa ujumla.
Balozi Msuya ambaye alimwandalia Mhe Spika chakula cha mchana, alimpongeza kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo mkubwa na kubainisha kuwa hatua hii imeiletea Tanzania sifa na heshima ya kipekee duniani kote. Aidha Balozi huyo ameipongeza Tanzania kwa kuendesha uchaguzi mkuu katika hali ya amani na utulivu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Spika Makinda kwenda nje ya nchi tangu achaguliwe kuwa Spika wa Bunge la Tanzania mapema wiki mbili zilizopita. Akizungumza na Balozi Msuya, Mhe. Makinda amesema kuwa nia yake kubwa ni kuwatumikia wabunge wote kwa haki na usawa pasipo kupendelea upande wowote.
“Bunge hili la kipindi changu linazo changamoto nyingi kwani linaundwa na watu wa itikadi na vyama tofauti. Ni wajibu wangu kutenda haki kwa kila mbunge kwa maendeleo ya taifa letu na kwa manufaa wa watanzania wote” alisema Spika Makinda.
Alipoulizwa kuhusu wabunge wa CHADEMA kutoka nje siku Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipolifungua Bunge rasmi, Spika alisema ni vema wabunge hao wakajua kuwa sasa uchaguzi umekwisha na ni vema wakaelekeza nguvu zao katika kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.
Akitolea mfano wa maridhiano ya Zanzibar na hatimaye kuundwa kwa serikali ya kitaifa, Spika Makinda amebainisha kuwa Tanzania inayo sifa ya kamaliza matatizo yake katika hali ya amani na maelewana na hivyo haamini kuwa suala la CHADEMA ni kikwazo kikubwa. Ni vizuri busara itumike ili warudi bungeni kuwatumikia wananchi, alisema.

Anaitwa ANNA MAKINDA na sio "ANNE" please waandishi wa kibongo msichakachue majina ya watu
ReplyDeleteOyaa na wewe umechapia, jina lake linaandikwa "Ana" siyo "Anna".
ReplyDeleteMama mkwe wangu huyo, ebo!
Jamani Ana na Anna ni mchakachuo wa Anne ambayo ndiyo spelling halisi ya jina hilo.
ReplyDeleteMnarumbana bure kwa mambo msiyoyajua. Jina ni hilihilo ila kila lugha ina matamshi yake na muundo wa kuliandika. Anna ni kwa kiingereza, Ana ni kwa Kiswahili na Anne ni kwa kifaransa. Mwenye jina ana uhuru wa kujiita atakavyo kwa kiingereza kwa kiswahili au kwa kifaransa. Ni sawa na ilivyo kwa John-kiingereza, Jean-Kifaransa. Vile vile Peter-kiingereza, Pierre-Kifaransa, Petro-Kihispania. Anthony-Kiingereza, Antoine-Kifaransa, Antonio-Kihispania. Au Claud-Kiingereza, Claude-kifaransa, Claudio-kihispania n.k
ReplyDeletemimi nimefurahia sana hiyo wine inayozalishwa tanzania pamoja na ukweli kuwa wenye kiwanda siyo watanzania ila inatoa matumaini kuwa we can. Mimi napena kuwakumbusheni kuwa dr shayo na team yake aliwahi kuyafanyia kazi sana tena kwa undani maswala ya masoko ya bidhaa za tanzania katika nchi 27 za ulaya. huu ni wakati wa kuangalia yale masoko na kujaribu kuuza bidhaa zetu huko. Tuacheni mambo ya kulumbana na majina!
ReplyDeleteSiku zooooete tunajua kuwa anaitwa anna makinda leo hii kawa spika wa bunge ndo mnajidai ati anne kwa kifaransa, mlikuwa wapi siku zote msimuite hivyo? tunajua majina mengi yapo kwa kiinglish, kifaransa nk, lakini mtu anaitwa jina lake halisi kutokana na jinsi alivyopewa jina na sio muanze sijui ni kwa kijapan haihusuuuu, tunajua anaitwa ANNA MAKINDA NA SIO ANNE FULL STOP!!
ReplyDelete