Sugu aongea mara baada ya matokeo kutangazwa.

a video hii na nyingine kibao BOFYA HAPA
Msimamizi wa kituo cha Chuo cha Uhasibu Bw. Samweli Lazaro jimbo la Mbeya Mjini amemtangaza Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu kupitia chama cha CHADEMA kwa kuibuka na kura 46,411 na kumbwaga mpizani wake CCM Bw. Benson Mpesya kwa kupata idadi ya kura 24,327.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mh. Joseph Mbilinyi. Mungu akusaidie ulitumikie taifa kwa uadilifu mkubwa. Akupe afya, nguvu na imani wakati ukiwa mgumu. Usisite kuomba ushari na kusikiliza ushauri.
    Tupo pamoja nawe, tuweke hii nchi sawa.
    Taji

    ReplyDelete
  2. Hiki ni kichwa halisi cha bongo flava na sio cha kudanganyiwa kutengenezewa studio!

    ReplyDelete
  3. Naona Ankal sasa hivi unamfagilia Sugu. Wakati wa kampeni ulikuwa huweki hata picha moja juu ya kampeni zake. Haya sasa, yeye tayari ni mheshimiwa, na wale wenzake walioamua kwenda kumpigia debe JK tuone watafika wapi.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana mkuu, tupo pamoja daima Sugu go....!!!

    ReplyDelete
  5. Watuu ........... maana ni ua garagaza ......... CCM chali kwa zaidi ya kura 22,000. Yap hiki ndio kizazi kipya ndani ya nyumba

    ReplyDelete
  6. Wat an equation Moshi mjini, arusha mjini mbeya mjini...SMART PEOPLE"

    ReplyDelete
  7. Yani hapa nipo na SUGU....tunacheza all night long ..... guess what RUGE MUTAHABA ndio DJ halafu KIBONDE ndio MC

    ReplyDelete
  8. hongera suguuuuuuuuuuuuuuuuu! acaha wale wachoka kiduku wale majani we ndani mujengoni! wanatamani kweli wakuite wakakufanyie intavyuu hapo klaus fm!

    ReplyDelete
  9. Big Up Mh Mr. II

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  10. lesson number one:dont underestimate anyone...ni hayo tu,jiwe hapa ukerewe

    ReplyDelete
  11. Ama kweli penye nia pana njia.. Hongera sana Sugu. Kama masikhara!

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Sugu, sasa wabonge wajue kwamba everything is possible waache kudanganyika kirahisi , watu wamechoka ! Sugu oyeeee! "yes we can"

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Mr Sugu.......Kila la kheri katika majukumu yako mapya........ulikuwa nyota katika fani ya Muziki uwe nyota katika kaiz hiyo.....nategemea hutakuwa kibaraka wa upande wowote zaidi haki na kweli.......

    ReplyDelete
  14. BİG UP SUGU , TUPO PAMOJA - WADAU UBATANİ

    ReplyDelete
  15. Mheshimiwa Sugu! Hongera sana! Walikuponda sana sasa Watakupongeza sana! Wape vidole viwili kuonysha pamoja tunalijenga Taifa letu lenye utajiri sana! Hakikisha ahadi zako zinapitiliza, Taji amesema ushauri omba na usilete usugu katika hilo man! Every1 is happy! Ebu toa single na Keputeni Komba mjengoni Dodoma basi-lol. Jamii iliyo na shida ni kutimiza malengo yake na sio porojo za mjengoni. Hakikisha unakumbukwa kwa mazuri. Ukiona unajisifia jana umefanya mazuri tambua leo hakuna kitu ulichofanya.

    ReplyDelete
  16. Hongera Sugu ..... mabadiliko yanatokana na sisi wenyewe , tukitaka inawezekana ,na ukiwa na dhamira , bidii na sababu unaweza

    ReplyDelete
  17. Watu walichonga sana. tena humu humu
    eti ohhh hapo wafuasi wako km wamejiandikisha utashinda kama hawajajiandikisha umekula mtama
    Sasa yuko juuuuuuuuu mheshimiwa wetu mpya mbeya mjini

    ReplyDelete
  18. Hongera Sugu pia hongera mheshimiwa John Mnyika! haya nia matokeo rasmi ya tume ya CCM. Sisi hatuwataki mtawale!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. Hongera sana wananchi wa Ubungo kuyabwaga mafisadi. Mnyika upo juuuuuu bado wanambania Mheshimiwa Mdee nafikiri muda si mrefu wataachia! Mafisadi wanatakiwa kusoma alama za nyakati! Usiibanie comment yangu wewe michuzi!

    ReplyDelete
  20. Kibonde endele akuchonga sasa! Anyway tunajua njaa zako ndizo zinakusababisha ujikombe kwa CCM muda wote

    ReplyDelete
  21. WANAKUITA SUGUUUU, WANAKUITA SUGUUUU, WANAKUITA SUGUUUU. HAPO DJ LAZIMA AWE RUGE MUTAHABA TU APENDE ASIPENDE.

    ReplyDelete
  22. Kaka Sugu Hongera Sana..4get wabaya wako wote wasije wakakutengenezea scandal wakuharibie we piga kazi wajali wapiga kura wako kwa kutimiza ahadi zako kuweka mazingira mazuri ya 2015.

    ReplyDelete
  23. mkandamizajiNovember 02, 2010

    braaaaaaaaap braaaaaaaaaap! Anti-Virus Mjengoni! Kudadadeki! Tunafagia virusi vyote vya ndani, tukimaliza tunafata vya nje!

    Big up kamanda way to go tunagonga mpaka isikike!

    Next 5 years: Rural Enlightment. Maana mjini wameshaamka!

    Pa1!

    ReplyDelete
  24. Mdau hapo juu kapteni Komba amepoteza ubunge hana lake tena. Kipindi hiki atumie kuangalia afya yake tu. Ha ha !!! muda wa mipasho umeisha watanzania tufanye kazi hatutaki bla bla !!! nyimbo kibao hamna utekelezaji kimekula kwaoooo!

    ReplyDelete
  25. daniel msemoNovember 02, 2010

    mheshimu kila mmoja anae hema na kutembea,mana hujui kesho atakua nani,na atakua wapi,so incouragin mh.sugu,salute,i knw u can n u'l make it,huku India tumefurahia ushindi wako sana!uliongoza hiphop.sasa tuongoze kulijenga taifa

    ReplyDelete
  26. Nyumba ya mafanikio ya Sugu, kulikuwa na Kamanda GSOLO. Hongera zako sana kuacha familia yako changa Dar na kuweka kambi Mbeya, ni imani yangu mtaendelea kusaidiana kimaisha, pia ni muhimu sana kuwasamehe wale wote waliowatosa maana hayo yamepita, sifa moja kuu ya kiongozi wa watu ni kuondoa makundi,washirikishe wabaya wako na wazuri wako kisha anza upya.

    ReplyDelete
  27. sugu sikia mafisadi walizoea stop sign now wamekutana na red light ukifika dodoma swali wataje wanakotoa hizo fedha umefika new york lent $1,500 bongo lent $3,000 kwa mwezi sema wajibu maswali hayo good luck brother

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...