Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Kilimanjaro stars,Mrisho Ngassa akionyesha umahiri wake mbele ya beki wa timu ya taifa ya Somalia katika mchezo uliopigwa leo ndani ya uwanja wa Taifa jijini.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Somalia mabao 3-0. Leo uwanja umejaa kwani kulikuwa hakuna kiingilio
Kiungo wa kati wa Kilimanjaro Stars,Henry Joseph akipena misuli na mchezaji wa timu ya Somalia katika mechi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliani wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars,Nurdin Bakari akipachika bao la tatu dhidi ya Somalia mara baada ya kupata krosi maridadi kabisa kutoka kwa Mrisho Ngasaa.hadi mwisho wa mchezo Kilimanjaro stars 3-0 dhidi ya Somalia.
Nyanda wa Somalia akifanyia msaada wa kuvishwa jezi mara baada ya kufanyiwa matibabu na mmoja wa matabibu waliokuwepo uwanjani hapo.
Kocha wa timu ya Kilimanjaro stars,Jan Paulsen akifatilia kwa makini mchezo huo.
Washabiki waliofurika katika uwanja wa Taifa leo wakishangilia mara baada ya kupatikana kwa bao la tatu la timu ya taifa ya Kilimanjaro stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. onea buji ,gombe gopa eeh?
    ngoja kiboko yenu Rwanda mtakiona

    ReplyDelete
  2. Hao wasomali mpaka wapate ajali ndio wafungwe? Wadau, hii timu inahitajika kunolewa zaidi. Aidha wazo la kuwa na timu za vijana litekelezwe, isiwe blabla tu. La si hivyo basi tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu/

    ReplyDelete
  3. Hapo mteremkooo, mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamuweziiiiiiiii...............!!

    ReplyDelete
  4. Mirungi na soka wapi na wapi? Msidhani soka letu limekuwa baada ya kuwafunga wala mirungi.

    ReplyDelete
  5. KIINGILIO ILIKUWA MIGUU YAKO NA MACHO YAKO. SAFI SANA NIMEIPENDA HII.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...