Jumuiya ya Watanzania UK (TANZ-UK) inayoandaa shughuli za sherehe za Uhuru wa Tanzania, inakaribisha maombi ya Mtanzania/Watanzania ya kuandaa chakula cha jioni cha Kitanzania.
Sherehe za Uhuru kwa Watanzania waishio hapa Uingereza itafanyika Jumamosi, tarehe 11/12/10 katika ukumbi wa Stratford Old Town Hall, Stratford, London. Balozi, Mh. Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. Watanzania watapata fursa ya kumkaribisha UK Balozi na familia yake siku hiyo.
Sifa za mwombaji wa tenda:
>Awe Mtanzania na uzoefu wa kupika kwenye sherehe yenye zaidi ya watu 100
Tafadhali tuma maombi yako kabla ya tarehe 30 Nov. 2010.
NB: Maombi yatakayofika baada ya 30/11 hayatapokelewa.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
Nelly Fungo simu namba: 07951320600
Nelly Fungo simu namba: 07951320600
au
nellyfungo@hotmail.com
Kwa taarifa zaidi ya shughulu hii tembelea tovuti ya Watanzania UK:
www.watanzaniauk.com/news
mobile no: 07424530228
email: tanzuk@ymail.com
website: www.watanzaniauk.com
Kwa taarifa zaidi ya shughulu hii tembelea tovuti ya Watanzania UK:
www.watanzaniauk.com/news
mobile no: 07424530228
email: tanzuk@ymail.com
website: www.watanzaniauk.com
Na kwa kiasi gani mnataka mpikiwe hicho chakula?
ReplyDeleteustadhi khamis wa leicester tenda hiyo kwa mheshimiwa balozi wa tanzania.
ReplyDeleteKwa nini awe Mtanzania?
ReplyDeleteJ. Mashaka
Kweli TA imepata viongozi...hata tenda zinaonekana kutangazwa siku hizi.
ReplyDeleteNinavyowajua Watanzania; watakao wasilisha maombi yao ya tenda watakuwa wachache sana 2 au 3 au hakuna atakayewasilisha kabla ya tarehe 30 Nov...!!! Wengi watasubiri kuja kulalamika na kupika majungu!!!
Mdau
London.
ONYO:
ReplyDeleteTUNAOMBA ILE TABIA YA KUTULETEA VYAKULA VYA KIHINDI KATIKA SHEREHE ZA KITANZANIA IKOME, MAANA NI AIBU KWANI MARA NYINGI MMEKUWA MKITUPIKIA CURRY VYAKULA VYA KIHINDI NA KIZUNGU WAKATI NI TUKIO LA KITANZANIA.
KWA NINI WATANZANIA TUNAJIAIBISHA KIASI HIKI? HATA WAGANDA, WANIGERIA, NK. WANATUSHINDA? WANAPIKA VYAKULA VYAO HADI UTAFURAHI KWENYE SHUGHULI ZAO.
TA TAFADHALI MTAKAYEMPA TENDA KWELI AWE ANAJUA NINI MAANA YA CHAKULA CHA KITANZANIA NA SI VINGINEVYO.
ASANTE TA KUTANGAZA TENDA.