Mbunge mtarajiwa wa Musoma Mjini Mh. Vicent Nyerere

Taarifa rasmi iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Musoma Mjini leo imethibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa CHADEMA kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge, Vedasto Mathayo Manyinyi wa CCM.


MATOKEO RASMI
Vincent Nyerere (CHADEMA) 21,335 (50.71%)
Vedasto Mathayo Manyinyi (CCM) 14,072 (39.38%)
Mustapha Juma Wandwi (Civic United Front) 253 (0.71%)
Chrisant Ndege Nyakitita (Democratic Party) 53 (0.15%)
Tabu Saidi Machibya (NCCR - Mageuzi) 19 (0.05%)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Chadema Oyee, Hongera sana Vincent Nyerere!

    Masha akubali kushindwa nyamagana. Tume itangaze matokeo. Amani isije potea nyamagana na Ilemela

    ReplyDelete
  2. Kama ndio mahesabu yenyewe hayo; 21,335(5.71 percent) na 14,072(39.38 percent), kuchakachua ni kazi jamani.

    ReplyDelete
  3. Vicent umetufanya wana Mara tujiskie very proud kwa siku ya leo.

    Nakutakia mafanikio mema.

    Uzomilye omsani wane :)

    ReplyDelete
  4. Nafurahi saana nikiona watoto wa Mwalimu wakiongoza kupigana dhidi ya ufisadi wa waoemu (wajiitao ccm)

    ReplyDelete
  5. Na Bado!!! tunakuja tu.

    ReplyDelete
  6. Jamani nahitaji kufahamu, kwani huyu ni mtoto wa mwalimu nyerere au ni nduguye, au ni majina tu yamefanana?

    ReplyDelete
  7. eeeeh naona wamechakachua weeeeeee lakini ikagoma na jamaa wanahasira sana wangeuwa watu hapa!

    ReplyDelete
  8. Lakini Vincent Nyerere ni nani? Jina lake anaitwa Nyerere, ndilo jina hasa la nyumbani ila baada ya ubatizo akapewa jina la Vincent. Baba yake ni Josephat Kiboko Nyerere, ambaye ni mzaliwa wa mwisho katika tumbo la Mgaya (Mama mzazi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere).

    Hivyo Mwalimu ni baba yake mkubwa tumbo moja na baba yake. Makazi yake ni Musoma mjini ambako ‘anajasiriamali’ katika kuusaka mkate wa kila siku.

    Vincent anasema, “Mimi hapo kabla ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa hadi tarehe 10/8/2008 ndipo niliamua kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
    “Kikubwa kinachofanya pia hatuendelei ni hawa wastaafu, ni serikali hiihii iliyoona sasa wamechoka na wanastahili kupumzika maana hata misuli na bongo zao hazifai kuhudumu tena, wakishapata kiinua mgongo wanafanya kazi upya kana kwamba hakuna vijana na wasomi wawezao kuifanya!”

    “Ni udhalilishaji, nasikia huwa wanawashikia nafasi watoto na wajukuu zao wakue ili kina Kayumba wasiingie hapo maana wataaibika na utendaji wa vijana maana wana machungu na nchi. Sasa ni hiari yetu kama tunataka maendeleo au la, kila kitu tayari sasa kilichobaki ni siasa safi na uongozi bora. Uongozi bora hauko CCM (japo wao wanaita utawala bora) maana vichwa vyao ni kutawala sio kuongoza”.

    ReplyDelete
  9. huoni wanavyofanana na Mwalimu na Maria pia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...