Taarifa rasmi iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Musoma Mjini leo imethibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa CHADEMA kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge, Vedasto Mathayo Manyinyi wa CCM.
MATOKEO RASMI
Vincent Nyerere (CHADEMA) 21,335 (50.71%)
Vedasto Mathayo Manyinyi (CCM) 14,072 (39.38%)
Mustapha Juma Wandwi (Civic United Front) 253 (0.71%)
Chrisant Ndege Nyakitita (Democratic Party) 53 (0.15%)
Tabu Saidi Machibya (NCCR - Mageuzi) 19 (0.05%)
Vincent Nyerere (CHADEMA) 21,335 (50.71%)
Vedasto Mathayo Manyinyi (CCM) 14,072 (39.38%)
Mustapha Juma Wandwi (Civic United Front) 253 (0.71%)
Chrisant Ndege Nyakitita (Democratic Party) 53 (0.15%)
Tabu Saidi Machibya (NCCR - Mageuzi) 19 (0.05%)
Chadema Oyee, Hongera sana Vincent Nyerere!
ReplyDeleteMasha akubali kushindwa nyamagana. Tume itangaze matokeo. Amani isije potea nyamagana na Ilemela
Kama ndio mahesabu yenyewe hayo; 21,335(5.71 percent) na 14,072(39.38 percent), kuchakachua ni kazi jamani.
ReplyDeleteVicent umetufanya wana Mara tujiskie very proud kwa siku ya leo.
ReplyDeleteNakutakia mafanikio mema.
Uzomilye omsani wane :)
Nafurahi saana nikiona watoto wa Mwalimu wakiongoza kupigana dhidi ya ufisadi wa waoemu (wajiitao ccm)
ReplyDeleteNa Bado!!! tunakuja tu.
ReplyDeleteJamani nahitaji kufahamu, kwani huyu ni mtoto wa mwalimu nyerere au ni nduguye, au ni majina tu yamefanana?
ReplyDeleteHongera.
ReplyDeleteeeeeh naona wamechakachua weeeeeee lakini ikagoma na jamaa wanahasira sana wangeuwa watu hapa!
ReplyDeleteLakini Vincent Nyerere ni nani? Jina lake anaitwa Nyerere, ndilo jina hasa la nyumbani ila baada ya ubatizo akapewa jina la Vincent. Baba yake ni Josephat Kiboko Nyerere, ambaye ni mzaliwa wa mwisho katika tumbo la Mgaya (Mama mzazi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere).
ReplyDeleteHivyo Mwalimu ni baba yake mkubwa tumbo moja na baba yake. Makazi yake ni Musoma mjini ambako ‘anajasiriamali’ katika kuusaka mkate wa kila siku.
Vincent anasema, “Mimi hapo kabla ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa hadi tarehe 10/8/2008 ndipo niliamua kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
“Kikubwa kinachofanya pia hatuendelei ni hawa wastaafu, ni serikali hiihii iliyoona sasa wamechoka na wanastahili kupumzika maana hata misuli na bongo zao hazifai kuhudumu tena, wakishapata kiinua mgongo wanafanya kazi upya kana kwamba hakuna vijana na wasomi wawezao kuifanya!”
“Ni udhalilishaji, nasikia huwa wanawashikia nafasi watoto na wajukuu zao wakue ili kina Kayumba wasiingie hapo maana wataaibika na utendaji wa vijana maana wana machungu na nchi. Sasa ni hiari yetu kama tunataka maendeleo au la, kila kitu tayari sasa kilichobaki ni siasa safi na uongozi bora. Uongozi bora hauko CCM (japo wao wanaita utawala bora) maana vichwa vyao ni kutawala sio kuongoza”.
huoni wanavyofanana na Mwalimu na Maria pia?
ReplyDelete