ARUSHA PRESS CLUB (APC)
P.O BOX 6011
ARUSHA, TANZANIA
TEL; 0713-231752 / 0754-299861
Email;arushapressclub@gmail.com


TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA (APC) JUU YA TUHUMA ZA WIZI WA LAPTOP KWA MWANDISHI MAGESA H. MAGESA.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), kinawajulisha waandishi wa habari mkoa wa Arusha, wadau na jamii kwa ujumla kuwa kina laani vikali kitendo kilichofanywa na mwandishi wa habari wa kujitegemea wa gazeti la Majira Magesa H Magesa kujaribu kwa nia ovu iliyo kinyume na misingi ya taaluna ya habari na sheria za nchi kuchukua LAPTOP isiyokuwa mali ya kwake kwenye semina ya Tanzania Public Health Association TPHA iliytofanyika Corridor Spring Hoteli mjini Arusha,Novemba 29,mwaka huu.

Kitendo hicho kimeidhalilisha, kimesikitisha na kimeiabisha tasnia nzima ya habari si mkoani Arusha tu bali nchi nzima kwa ujumla wake. Hivyo basi APC kinapenda kuomba radhi kwa wadau wote walioguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.

Ieleweke kwamba APC haihusiki kwa namna yoyote ile na uovu uliokithiri wa baadhi ya waandishi wa habari na kamwe haitafumbia macho masuala kama hayo.

Kwa mujibu wa Katiba yake, APC itawatetea, kuwalinda na kuwapigania wanachama wake watakao nyanyaswa, kuonewa na kubugudhiwa wakati wa utendaji wa shughuli halali za kitaaluma na nyingine za kijamii na si vinginevyo.

Kwa misingi hiyo basi, na kwa kufuata Katiba ya APC, Kamati Kuu ya APC baada ya kupokea taarifa hizo na kujadili kwa kina tukio hilo ovu,na kwa kutumia kipengele cha 3 (c) cha Mamlaka na mipaka ya Kamati ya Haki,meamua kusitisha uanachama wa Magesa H. Magesa kwa muda hadi hapo uchunguzi wa tukio hilo, unaohusisha vyombo vya dola, utakapokamilika.

Katika kipindi hicho Magesa H. Magesa amevuliwa uanachama wa APC kwa mujibu wa Katiba ya Chama, na hata ruhusiwa kujihusisha na jambo lolote linalohusiana na APC.

APC inapenda kuchukua nafasi hii kuwaonya wanachama wake wenye tabia zinazokinzana na uandishi wa habari,na zenye dalili za makosa ya jinai kuwa haitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watakaothibitika kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama kwa mujibu wa Katiba.

Aidha, APC inawaomba wadau wote wa sekta ya habari mkoani Arusha kutoa ushirikiano wa dhati kwa APC ikiwa ni pamoja na kuwaripoti chamani mara moja waandishi wote watakao kuwa na tabia hizo ikiwa ni pamoja na wale wanaovamia mikutano, semina na shughuli nyinginezo bila ya kualikwa.

Daima tutashirikiana na wadau wote wa habari katika kuhakikisha kuwa fani ya uandishi wa habari mkoani Arusha inaboreshwa kwa manufaa ya jamii nzima

Eliya Mbonea
Katibu Mkuu-APC

December 2, 2010
Nakala .
UTPC
RPC -Arusha
RC -Arusha
DC -Arusha
MCT
Gazeti la Majira
Jukwaa la Wahariri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Niliibiwa simu na waandishi wa habari wa arusha december mwaka jana. Nilikuwa nawapa briefing ya workshop niliyo iandaa pale golden rose. Wakanizunguka wengi kweli wenye mike hayaaa, wenye kamera hayaaaa, wenye kalamu hayaa nikafurahi kweli kuona kuwa sekta ya habari imekuwa nchini and in a way, what I was saying was sensible. Lo and behold! before I knew it simu yangu kwishney! Nilisikitika sana lakini nimewasamehe. Ni njaa.

    ReplyDelete
  2. Eh! bwana Michuzi, kama vipi mimi najitolea kumnunulia lap top huyu mwandishi; hii ni aibu at!

    ReplyDelete
  3. A strong statement and a warranted one IF the man is arraigned and found guilty in a court of law. But at the moment it seems premature and condemnatory since the matter is under investigation and the man has yet to be charged.

    ReplyDelete
  4. Wanahabari tunawategemea sasa wanatuangusha miaka kama minne kunamwandishai mmoja wa Arusha aliazima Video Camera ndogo ni nzuri tu kwasababu mwandishi na tumemzoea ajairudisha mpaka leo hii na tumempigia simu mara nyingi akamua kubadilisha line ya simu tukamfuata ofisini kwake akituona anatutoroka mpaka sasa tumejamaza tu tunamuangalia akiriport kwenye vyombo vya habari tunaona ni mwizi tu sasa waandishi wa Arusha tuwaweke kundi gani mnatia aibu jirekebisheni tafadha sisi tunawapenda

    ReplyDelete
  5. Pia kuna tabia ya kuvamia warsha mbali mbali na kuannza kuvamia misosi kama vile wametoka GOMA

    ReplyDelete
  6. niliwahi kupiga kelele sana juu ya tabia chafu za baadhi ya waandishi wa habari wa jiji la arusha,nikaonekana mbaya sana siwatakii mema,pamoja na hayo nikawashawishi kuwa macho na waandishi wenye tabia hizo bado nikaonekana wabaya,ni hawhawa waloiwahi kufungiwa impla hoteli jikoni baada ya kula msosi kwenye mkutano mwaka juzi bila ya mwaliko,haya bwana hayawi hayawi yamekuwa umleavyo ndivyo akuavyo

    ReplyDelete
  7. JIVI NYIE WAANDISHI MBONA HAMJUI KISWAHILI? Fri Dec 03, 04:02:00 AM
    AMEANDIKA SEKTA YA HABARI IMEKUWA!Fri Dec 03, 07:53:00 AM AMEANDIKA AJAIRUDISHA! HII INANIKUMBUSHA FILAMU MOJA INAYOITWA UWA LA WARIDI! JAMANI HAYA SI MAKOSA YA UCHAPAJI BALI KISWAHILI CHETU NDIVYO KILIVYO, KAMA WAZIRI ANAWEZA AKASEMA ZAHABU ZETU TENA NDANI YA BUNGE NA AKAPIGIWA MAKOFI!

    ReplyDelete
  8. nafikiri kumsimamisha kwa muda kusubiri uamuzi wa kisheria ingekuwa busara badala ya kuandika public speeches na kutoa lawama na kukemea kitu ambacho hakijathibitishwa. ningekuwa mimi, nikionekana sina hatia, nawafungulia kesi kwa defamation. dhalilisho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...