TAIFA STARS IMETWAA UBINGWA WA KOMBE LA TUSKER CECAFA CHALLANGE CUP BAADA YA KUIDUNGUA IVORY COAST 1-0 KATIKA MCHEZO WA FAINALI WA MICHUANO HIYO ILIYOMALIZIKA SASA HIVI NESHNO JIPYA JIJINI DAR.
MFUNGAJI WA BAO HILO NI NAHODHA SHADRACK NSAJIGWA KWA NJIA YA PENATI BAADA YA BEKI WA IVORY COAST KUUNAWA MPIRA KWENYE DAKIKA YA 31.
UWANJA UMELIPUKA KWA NDEREMO NA VIFIJO HIVI SASA NA WAKATI WOTE WAZIRI WILLIAM LUKUVI AMBAYE NI MGENI RASMI ATAKABIDHI KOMBE NA ZAWADI KWA WASHINDI.
MSHINDI WA TATU NI UGANDA AMBAYO IMEIFUNGA ETHIOPIA KWENYE MCHEZO WA AWALI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. MAGANGA FERUZIDecember 12, 2010

    ANKAL.
    ASANTENI WATANZANIA KWA DUA NA SALA ZENU. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI KILIMANJARO STARS.
    TUMESUBIRI SANA KWA MIAKA 16 HATIMAYE TUMESIMAMA.

    MAGANGA FERUZI

    ReplyDelete
  2. big up uncle michu!!!!!
    big up paulsen!!!!
    big up Nsajigwa!!!!
    big up JK!!!!
    big up wachezaji wote!!!!!
    big up Jimmy Kabwe!!!!!
    big up Musonyi!!!!! na mwakani nchi itakayoshindwa kuandaa tuleteeni ten tunuchukue!!!!
    mdau
    chapaulaya
    Sweden

    ReplyDelete
  3. SAAFI SANA SAAFI SANA. SASA SISI SIYO TENA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KILA ANAYETAKA KUNYOA AJIFUNZIE KWETU. HILO SASA LIMEKUA HISTORIA.

    ReplyDelete
  4. well done boys, Excellence should be our bench mark .... mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  5. Asalaama alaykhum Ankal,

    Nilikua naangalia mpira Online kwa kupitia supersport nimefurahi sana USHINDI WA TIMU YA TAIFA, Alfani Ngasa,Juma Kaseja na Shadrack Nsajigwa Mashujaa wetu wameibeba sana timu kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

    Mechi ya leo tungeweza funga magoli mengi sana pengo la Ngasa limeonekana. Upande wa mabeki kwakweli wapo fiti si mchezo wanapiga kazi hasa.

    "MUNGU IBARIKI TANZANIA"

    Wasalaam

    Chef Issa

    ReplyDelete
  6. hongera sana vijana kwa juhudiza kuchua kombe hilo hongereni sana mdau hydrabad

    ReplyDelete
  7. Mh Michuzi Assalaam Aleykhum.
    Hongera watanzania wote,Zaidi kabisa ni kwamba TFF mujiangalie upya. Mlionyesha uungwana kuwezesha watazamaji kuangalia bure. Mpira na nguvu ya wananchi kushangiria kwa nguvu huenda pamoja kuleta ushundi. Ushindi ni gharama lazima mpate hasara kabla ya kuanza kuingiza faida. Sasa wananchi wakijenga imani na Timu yetu hatutashindwa kulipa viingilio.
    Mungu ibariki Tanzania,viongozi na watu wake

    ReplyDelete
  8. Ni Mrisho Ngassa sio Alfan Ngasa japo hajacheza leo,mkubwa mpira tumeuona huku ughaibuni vijana wamechukua kombe hongera sana ila bado kimpira tupo nyuma sana hatujajitahidi kutandaza lakini ndio kombe tunalo sasa zaidi ya miaka 15 Maximo alijitahidi kutengeneza ukuta mgumu na hilo linaonekana sasa ni kazi ya Paulsen kutengeneza fowadi ambayo bongo hakuna labda tufosi kuwanoa Ngasa,Boko na tegete halafu vipi Mgosi?
    Misho ushauri wangu ni muhimu sana kuwa na kocha mzawa kwani tatizo ni lugha kwa wachezaji wetu.
    Kenya wana Mzawa Mulee(japo kajiuzulu),Uganda wana mtasha na waganda lugha ipo poa,Ivory wana mfaransa na Misri wana Shehata inakuaje bongo mdenish na wachezaji wanaishia kusema british smoke a chair?

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  9. drogba hakuwemo

    ReplyDelete
  10. si lazima mseme mmeangalia kupitia wapi tunajua mpo majuu.HAYA KWA TAARIFA ZENU GAME ILIPANGWA.

    ReplyDelete
  11. Hii Ivory Coast ilikuwa timu ipi maana nimemwona Drogba na Kalou wakichezea Chelea leo and akina Toure wakichezea Man City jana. Pia sidhani kama akina Eboue and wengine walikuwepo. Itakuwa ni timu B au?

    ReplyDelete
  12. Mdau uliyesema tatizo ni kiingereza nakuunga mkono, ila tatizo kubwa la wachezaji wetu ni nidhamu. Hata akaletwa kocha mzawa (Mkwere, mziguz, mpzre ama mchaga hata mmakonde)bila kimarisha suala la nidhamu bado tatizo litakuwa pale pale.

    Mpiga Box (MPG Bx)

    ReplyDelete
  13. Jamani timu ilishinda sio timu ya tanzania ni timu ya taifa ya tanganyika!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. kwa mdau wa Sun Dec 12, 08:59:00 PM wewe si mpenzi wa mpira na hujui lolote kuhusu mpira, maana kama unajua usingelisema ulilolisema.

    ReplyDelete
  15. Haya waosha vinywa matunda ya JK hayo yanaonekana, na bado timu ya wanawake, na michezo mingine, waimba bongo fleva kama kina Ali Kiba wacheza sinema za bongo, zote hizo ni ajira.

    ReplyDelete
  16. Annon wa 09:16 hapo juu acha ama ushamba au hujui ulizungumzalo watu hawataki kuelezea kama wapo majuu au machini wanajaribu kuweka mada zao hapa lengo likiwa kuchangia kama watanzania wengine,acha gere za kizamani kwani wa majuu na wa machini wote si watanzania?kuhusu game kupangwa hiyo ni falsafa yako ya kizamani ambayo nafikiri upo umuhimu wa kuchunguzwa ikiwezekana ukaisaidie kamati ya CECAFA uonyeshe nani aliyepanga game hiyo.

    We mkubwa sasa na fahamu hii ni blog ya jamii kama huna la kuzungumza basi bora ufanye lingine la maana.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  17. fair due, timu ya taifa iliyoshinda ni timu ya taifa ya tanganyika na sio timu ya taifa ya tanzania, fact........

    ReplyDelete
  18. ...Furaha tuliyoikosa kwa miaka zaidi ya 15..imerudi ghafla...K.Stars mmenifurahisha sana! Najua hadi mwakani tena mtakuwa mmeshajifua zaidi ya kiwango...wembe uwe mkali zaidi...Nyoa nyoa woote..sijui the Cranes..Warundi, wa-Chipolopolo..Harambee..wote nyoa kabisa mwakani. Mungu ibariki Tz...Mungu ibariki K.Stars..na Mungu wabariki mashabiki pia..
    Mdau-Manchester, UK

    ReplyDelete
  19. Kwa kweli kwa hali hii nampongeza sana jk maana yeye ndie ambaye amekuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha kocha anapatikana na hasa wa nje maana jamanani makocha wa tz itakuwa wachezaji mazoea mengi sababu ya kiswahili.

    ReplyDelete
  20. Naungana na anon aliyesema jk anahitaji sifa. big up. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

    ReplyDelete
  21. Mdau wa Dec 12, 09:16pm acha kuendeleza malumbano kati ya wanuka vikwapa na wabeba mabox. Sisi wabeba mabox tuliuangalia huo mpira, kuhusu wapi, its none of your MF business. Nyie wanuka vikwapa mnapenda sana kutusakama sijui mnadhani kwa kuwa mpo bongo ndio mnaown kila kitu. Mada hapa ni ushindi, wote tumefurai na tunawapongeza watanzania wote, wachezaji na Viongozi wetu.

    ReplyDelete
  22. Bongo na Kilimanjaro Aireeeeeeeeeeeeeeeee tusonge mbele daima hongera saaaaaana.

    ReplyDelete
  23. Sijui kama Maximo ALIIIONA HII GAME MAANA kASEJA KAMZODOA KWA VITENDO, Kocha miaka minne hana hata First Eleven, watu mlisemama ooh Poulsen Kibabu sasa kawaonbyesha yeye ana level ya namna gani, Bravooo Kilimanjaro, RIP Mziray, Bambaga

    ReplyDelete
  24. Your facts are true. Team iliyoshinda ni timu ya Tanganyika. Zanzibar Heros walitolewa. Congratulations

    ReplyDelete
  25. We Zanunu(Anony 12 Dec: 08:36:00) ''please smoke the chair' = Naomba uvute ( usogeze) kiti'' ndo wachezaji wetu wasemavyo?, du! mie mbavu sina.

    Hongera Tanganyika stars.

    Mdau
    Mai

    ReplyDelete
  26. Wewe ( Mon Dec 13, 04:18:00 AM, ) utakuwa ni A/BBC (Tafuta maana yake huko)mpuuzi mkubwa unaita watu wanuka vikwapa!!?? wewe nani hasa? *(&*%^%^()*(*^%%$ zako

    ReplyDelete
  27. Kumbe inauma mkiitwa wanuka vikwapa, Lakini nyie kuita watu wabeba mabox ni poa tena raha. Kuhusu "A/BBC" who cares? wote ni watanzania hakuna haja ya kuitana majina ya kashfa.Kama wote tukiamua kuishi bongo, basi hapatatosha. No body is better than others!!!

    ReplyDelete
  28. MAXIMO hakufanya lolote la maana muda wake wote aliokuwepo nchini, we kocha gani kwa miaka 4 alishindwa kuleta hata kombe la challenge, kila siku anafukuza wachezaji na kuweka wachezaji wa hovyo timu haina hata formation. MAXIMO hakuwa hata na historia ya kufundisha timu yoyote ya maana. Huyu Mzee Poulsen alikuwa kocha wa pili wa timu ya taifa ya Denmark anaonekana tu ana ujuzi na kuwajua wachezaji hata mabadiliko yake huzaa matunda kama alivyo Furgason wa Man U. Marehemu Mziray alikuwa anaonesha waziwazi ubovu wa Maximo, angekuwa hai angeweza kuthibitisha yale aliyokuwa akiyasema siku zote (RIP) Mziray na Hongera Kaseja mtumie salamu Maximo kilaza wa makocha.

    ReplyDelete
  29. TIMU YETU INA VIPAJI KAMA ZILIVYO TIMU ZA NCHI NYINGINE ASIKWAMBIE MTU. TATIZO TULIKUWA HATUNA KOCHA TU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...