Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza
Marehemu Abou Semhando (kulia, fulana nyekundu) akiwa katika mazishi ya Dk. Remmy Ongala na wakongwe wenzie. Toka shoto ni Mzee Makassy, Tschinga Kalala Assosa, King Kikii na Kanku KellyNa John Kitime
Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.
Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.
Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake.


jamani kapumzike kwa amani baba Diana, wapenzi wa twanga tumepoteza shujaa
ReplyDeleteinalilahi wainailahi rajiuun
ReplyDeletepoleni wafiwa
Oh maskini Abou Mola akulaze pema peponi...hii ni pigo tena kubwa...
ReplyDelete/Mdau Vumbi Dekula Sweden
Inna Lilahi wa inna illahi R.I.P Abou
ReplyDeleteR.I.P Semhando,tutakukumbuka daima.
ReplyDeleteWahenga walisema hakuna msiba usio na mwenzie. Huyu kamsindikiza Dr. Remmy Ongala ... wote ni waimbaji wa muziki wa dansi.
ReplyDeletepikipiki za mchina jamani zinatuondoshea watu wetu , usikute hapo asilimia kubwa ya ajali hiyo ni pikipiki ya mchina ....
ReplyDeletendo maana mimi pikipiki nina allegy nazo..
poleni wafiwa
R.I.P Abuu Semhando
ReplyDeleteRest In Peace Baba Diana.
ReplyDeleteno please!no sielewi ninachokisoma
ReplyDeleteau naota? no please!!! noooooooooo
Rest in the eternal peace.Tuwe tayari wakati wowote maana hatujui siku wala saa.
ReplyDeletePOLENI SANA TWANGAPEPETA WOTE
ReplyDeleteR.I.P ABUU.
ReplyDeleteDAIMA TUTAKUKUMBUKA.
INNA LILAH WAINA ILAIHI RAJEUNN
ReplyDeleteKwaheri baba Diana..kapumzike kwa amani..wapenzi wa twanga inogile tutakukosa sana.Amen
ReplyDeletenaona serikali ingepunguza bei za magari ili tuachane na hizo pikipiki!!zitatumaliza!!!
ReplyDelete