Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza
Marehemu Abou Semhando (kulia, fulana nyekundu) akiwa katika mazishi ya Dk. Remmy Ongala na wakongwe wenzie. Toka shoto ni Mzee Makassy, Tschinga Kalala Assosa, King Kikii na Kanku Kelly
Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime

Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.

Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.


Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.


Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. jamani kapumzike kwa amani baba Diana, wapenzi wa twanga tumepoteza shujaa

    ReplyDelete
  2. inalilahi wainailahi rajiuun

    poleni wafiwa

    ReplyDelete
  3. Oh maskini Abou Mola akulaze pema peponi...hii ni pigo tena kubwa...
    /Mdau Vumbi Dekula Sweden

    ReplyDelete
  4. Inna Lilahi wa inna illahi R.I.P Abou

    ReplyDelete
  5. R.I.P Semhando,tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  6. Wahenga walisema hakuna msiba usio na mwenzie. Huyu kamsindikiza Dr. Remmy Ongala ... wote ni waimbaji wa muziki wa dansi.

    ReplyDelete
  7. pikipiki za mchina jamani zinatuondoshea watu wetu , usikute hapo asilimia kubwa ya ajali hiyo ni pikipiki ya mchina ....

    ndo maana mimi pikipiki nina allegy nazo..

    poleni wafiwa

    ReplyDelete
  8. R.I.P Abuu Semhando

    ReplyDelete
  9. Abiola Jr. New Albany OhioDecember 18, 2010

    Rest In Peace Baba Diana.

    ReplyDelete
  10. no please!no sielewi ninachokisoma
    au naota? no please!!! noooooooooo

    ReplyDelete
  11. Rest in the eternal peace.Tuwe tayari wakati wowote maana hatujui siku wala saa.

    ReplyDelete
  12. POLENI SANA TWANGAPEPETA WOTE

    ReplyDelete
  13. R.I.P ABUU.

    DAIMA TUTAKUKUMBUKA.

    ReplyDelete
  14. INNA LILAH WAINA ILAIHI RAJEUNN

    ReplyDelete
  15. Kwaheri baba Diana..kapumzike kwa amani..wapenzi wa twanga inogile tutakukosa sana.Amen

    ReplyDelete
  16. naona serikali ingepunguza bei za magari ili tuachane na hizo pikipiki!!zitatumaliza!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...