Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal kushoto, akimfariji Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya pili Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, kutokana na kifo cha Mtoto wake Suleiman Aboud Jumbe kilichotokea mwishoni mwa wiki hii Nchini India, wakati Makamu wa Rais alipohudhuria Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Mzee Jumbe Migombani mjini Zanzibar jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal kushoto, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katikati na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wasoma Dua ya pamoja kwenye Mazishi ya Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe, yaliyofanyika nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifukia kaburi kwenye mazishi ya Mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, yaliyofanyika nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar jana jioni. Picha na mdau Amour Nassor wa VPO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. iNNALLILLAH WAINNA RRAJIUUN.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa. Mzee Aboud Jumbe alikuwa ni kiongozi mzalendo na mwadilifu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...