Mbunifu nguli Manju Msita akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar. Shoto ni Meneja Masoko wa Swahili Fashion Week, Hamisi Omary
Juu na chini ni ubinfu wa Manju Msita
UHUSIANO KATI YA SWAHILI NA
MOZAMBIQUE FASHION WEEK WAIMARIKA

Ni awamu ya sita kwa tamasha kubwa la kila mwaka Mozambique fashion week litakalofanyika kuanzia tarehe 6-11 Disemba mjini Maputo Msumbiji. Mahusiano kati ya Swahili na Mozambique fashion week yalianza mwaka 2009 kwa washiriki Adelia na Sheila Tique kuiwakilisha Msumbiji katika Swahili fashion week 2009 na baadaye Swahili fashion week iliwakilishwa na Jamira Vera Swai.

“Mwaka huu Marinella Rodriguez aliiwakilisha Mozambique Fashion Week katika Swahili fashion week, kwa heshima na furaha kubwa tunajivunia kumchagua Manju Msitta kuiwakilisha Swahili fashion week katika tukio muhimu mjini Maputo siku ya tarehe 11 Disemba” alisema Mustafa Hassanali muanzilishi wa Swahili Fashion Week.

“Ni furaha kubwa kuiwakilisha Tanzania na Swahili fashion week katika maonesho ya Mozambique Fashion Week mwaka huu. Nina imani nitaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania na Afrika mashariki katika tukio hili la kidunia.” Alisema Manju msita

Manju alichaguliwa na muandaaji wa maonesho ya mavazi wa kimataifa Jan Malan Umzingeli kwa kushirikiana na Swahili Fashion Week kwa kigezo kwamba kazi zake zina kiwango cha juu kulingana na ubora wa ubunifu wa mavazi yake.

“Huu ni mwanzo wa kuimarisha mahusiano baina yetu, na sio siasa pekee inayotuunganisha Tanzania na Msumbiji ila kupitia Utamaduni pia unatuunganisha.Uhusiano huu uendelee zaidi na kuwa imara mwaka hadi mwaka.” aliongeza Hassanali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. All the best Manju. Enjoy Maputo!

    Mteja Sugu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...