Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Lazaro Nyalandu, akiweka saini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Ya Ludewa,Bi. Hilda Lauwo ( Aliyesimama). Nyuma ya Naibu Waziri ni Mbunge wa Ludewa Mh. Deo Filikunjombe
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akipata maelezo ya awali kutoka kwa Mbunge wa Ludewa Deogratius Filikunjombe ( kushoto) na Msimamizi wa Mradi wa Liganga/Mchuchuma, Bw. Lawrence Manyama.(Kulia)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akihojiwa na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vilivyoshiriki katika ziara yake.
Haya sio mawe, ni chuma cha Liganga kikiwa juu kabisa ardhi. Eneo la takriban km za mraba 140 zimetapaa madini haya kuanzia chini ardhini hadi juu katika uso wa ardhi. Kuendelezwa kwa mradi huu kunatajwa kuwa suluhisho la hujma dhidi ya miundo mbinu yetu kunakofanywa na wahalifu ili kupata chuma chakavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Jamani Mawaziri na Manaibu wenu mnapoanza ziara za kikazi nikiwa na maana za kiserikali kwepeni kuvaa vitambulisho vya U-CCM. mnawafanya watu wa itikadi nyingine kuona kama bado ni kampeni zinaendelea. Mko kulitumikia Taifa na vyema mkawa wa kawaida kabisa.
    Chapeni kazi uchaguzi umeisha mmeshakabidhiwa dhamana hizo sare zisubiri wabunge wasio mawaziri na ninyi hadi 2015 kama mnaona itafaa;

    Mdau

    ReplyDelete
  2. yupo wapi yule wifey wake Miss Tz? Au ashamchoka?
    Mbeya kuna vitu vinono, malizana na makaa ya mawe kwanza!

    ReplyDelete
  3. Wow nimekubali Mbeya kuna vitu vinono haswa me mwenyewe shahidi..!!
    Mhn. huko juu, tulikuW wote hapa tunapiga box sasa hivi huko juu wangu...!!!!

    ReplyDelete
  4. Hongera Mh Nyalandu. Combination yenu pale wizara ya Viwanda ni ya kipekee, Waziri Kichwa, Naibu kichwa, Fanyeni kazi sasa. Natamani huo umeme wa makaa ya mawe uwake leo tuepukane na adha ya mgao

    ReplyDelete
  5. Hongera Mh Nyalandu. Combination yenu pale wizara ya Viwanda ni ya kipekee, Waziri Kichwa, Naibu kichwa, Fanyeni kazi sasa. Natamani huo umeme wa makaa ya mawe uwake leo tuepukane na adha ya mgao

    ReplyDelete
  6. Hivi NDC ipo hai au imekufa? Nyalandu na Chami ifufueni kwa kuipa funds na watendaji makini ili hayo mazuri ya Liganga na Mchuchuma yatufikie Watanzania

    ReplyDelete
  7. Hivi NDC ipo hai au imekufa? Nyalandu na Chami ifufueni kwa kuipa funds na watendaji makini ili hayo mazuri ya Liganga na Mchuchuma yatufikie Watanzania

    ReplyDelete
  8. Tanzania ina neema za ajabu, Wizara ya Viwanda tangazeni mambo haya. Sisi tulioko nje tunawajua watu wenye hela zao za kuweza kuwekeza lakini taarifa hazipatikani

    ReplyDelete
  9. Nyalandu ni kichwa kweli, hakutakiwa kuwa waziri ili awajibike kwa Taifa badala ya CCm, any way endeleza uzalendo

    ReplyDelete
  10. Ni taarifa njema sana

    ReplyDelete
  11. Tanzania bwana, tuna kila sababu ya kuwa juu sana kiuchumi, tastizo ni taarifa. Ziko wapi taarifa za tafiti kama hizi za makaa ya mawe? Tutajuaje faida bila kuambiwa na wahusika? Itikieni wito wa Rais Mstaafu Mkapa na Huyu wa sasa JK, wanataka mtoe habari sio kuzilalia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...