Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando, Kasaloo Kyanga, Fan Fan

Ratiba ya Mazishi ya mwanamuziki na na meneja wa Bendi ya African Stars-Twanga Pepeta Marehemu Abou Ally Semhando “Baba Diana”

· Jumamosi ndugu na jamaa walikusanyika nyumbani kwa marehemu, Mwananyamala Kisiwani(Ngilangwa) kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

· Leo Jumapili 19/12-Saa11 baada ya Swala ya alfajiri katika msikiti wa Muhimbili, waombolezaji kuingia katika magari na kuelekea kijiji cha Kibanda, Muheza tayari kwa mazishi.

· Mara baada ya chakula cha mchana mwili kupelekwa msikiti wa Muheza nabaada ya swala mwili kupelekwa makaburini kwa maziko.

· Waombolezaji watarejea Dar es Salaam baada ya maziko.

Hakika Msiba wa Abou unaumiza sana

1. Jumamosi ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba likizo
3. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.

4. Alikuwa mpiga drum wa Dk. Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka mwaka 1981

-John Kitime


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwa kweli hata mimi Baba Di ameniumiza sana mno! Mungu amuweke mahali pema sote tuko nyuma yako. Upumzike kwa amani. Kweli dunia ni uwanja wa fujo sijui ni Juwata waliimba, wengine wanafurahia mama amepata mtoto wengine wanahuzunika mtoto wao kagongwa leo, hebu utafuteni huo wimbo tuusikilize

    ReplyDelete
  2. Inna Lilahi wa inna illahi rrajuyn
    hakika kila nafsi itaonja umauti poleni sana ndugu wafiwa na sisi mashabiki wa Twanga na kupepeta

    ReplyDelete
  3. R.I.P BABA DIANA
    DAIMA TUTAKUKUMBUKA
    MPILI MPILI

    ReplyDelete
  4. Mdau, MalaysiaDecember 19, 2010

    R.I.P Baba Diana,
    mchapakazi mahiri na aliyejituma. MAshabiki wako wa Twanga tutakukumbuka sana.
    Ulale kwa amani.

    ReplyDelete
  5. kuamini inakuwa ngumu jamani masikini ametoka kumzika mwenzie remmy bila ya kujua na yeye anamfuata yn inauma zaidi pale kufa na uzima wake bora ata angeumwa useme kaumwa lkn ajali hz jamani kweli tunatembea na vifo mkononi lol ujui siku wala saa inauma sanaaa poleni sn wafiwaaa

    ReplyDelete
  6. RIP Baba Diana.
    Waziri anayehusika na mambo hayo kulikoni wajameni?

    ReplyDelete
  7. poleni sana wafiwa wote.
    R.I.P BABA DIANA
    DAIMA TUTAKUKUMBUKA
    MPILI MPILI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...