Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando, Kasaloo Kyanga, Fan Fan
Ratiba ya Mazishi ya mwanamuziki na na meneja wa Bendi ya African Stars-Twanga Pepeta Marehemu Abou Ally Semhando “Baba Diana”
· Jumamosi ndugu na jamaa walikusanyika nyumbani kwa marehemu, Mwananyamala Kisiwani(Ngilangwa) kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wafiwa.
· Leo Jumapili 19/12-Saa11 baada ya Swala ya alfajiri katika msikiti wa Muhimbili, waombolezaji kuingia katika magari na kuelekea kijiji cha Kibanda, Muheza tayari kwa mazishi.
· Mara baada ya chakula cha mchana mwili kupelekwa msikiti wa Muheza nabaada ya swala mwili kupelekwa makaburini kwa maziko.
· Waombolezaji watarejea Dar es Salaam baada ya maziko.
Hakika Msiba wa Abou unaumiza sana
1. Jumamosi ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba likizo
3. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.
4. Alikuwa mpiga drum wa Dk. Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka mwaka 1981


Kwa kweli hata mimi Baba Di ameniumiza sana mno! Mungu amuweke mahali pema sote tuko nyuma yako. Upumzike kwa amani. Kweli dunia ni uwanja wa fujo sijui ni Juwata waliimba, wengine wanafurahia mama amepata mtoto wengine wanahuzunika mtoto wao kagongwa leo, hebu utafuteni huo wimbo tuusikilize
ReplyDeleteInna Lilahi wa inna illahi rrajuyn
ReplyDeletehakika kila nafsi itaonja umauti poleni sana ndugu wafiwa na sisi mashabiki wa Twanga na kupepeta
R.I.P BABA DIANA
ReplyDeleteDAIMA TUTAKUKUMBUKA
MPILI MPILI
R.I.P Baba Diana,
ReplyDeletemchapakazi mahiri na aliyejituma. MAshabiki wako wa Twanga tutakukumbuka sana.
Ulale kwa amani.
kuamini inakuwa ngumu jamani masikini ametoka kumzika mwenzie remmy bila ya kujua na yeye anamfuata yn inauma zaidi pale kufa na uzima wake bora ata angeumwa useme kaumwa lkn ajali hz jamani kweli tunatembea na vifo mkononi lol ujui siku wala saa inauma sanaaa poleni sn wafiwaaa
ReplyDeleteRIP Baba Diana.
ReplyDeleteWaziri anayehusika na mambo hayo kulikoni wajameni?
poleni sana wafiwa wote.
ReplyDeleteR.I.P BABA DIANA
DAIMA TUTAKUKUMBUKA
MPILI MPILI