Mpendwa Mjomba Michuzi,
Habari za kazi Mjomba, nimevutiwa sana na picha hii ambayo mama mmoja aliyekuwa anakatiza mitaa ya Tukuyu mjini mchana huu maeneo ya Stendi kuu akiwa amembeba kuku Jogoo mithili ya mtoto mgongoni kwa kumfunga kwa mbeleko. Hii inaonesha ni jinsi gani mama huyu anawajali viumbe vingine. Sifa tele kwake na wengine tuige.
Wasalaam,
Mjomba Juma, Tukuyu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hakuna upendo ni kitoweo tu hicho babake

    ReplyDelete
  2. duh watu weusi vituko !!

    ReplyDelete
  3. we unayesema watu weusi vituko, je wale wenye rangi nyingine hujasikia vituko vyao?
    1. kulala na mbwa
    2. kulamba kinyeo na kazalika.

    huyo mama kabeba kuku kurahishisha mambo badala ya kumning'iniza kichwa chini - kwanza inachosha mikono na (sijui kama alikuwa anawazia haki za wanyama) lakini kampa nafuu kubwa sana huyo jogoo

    ReplyDelete
  4. mmm...nievunjika mbavu.....kweli blogg inatupa rahaa....na aliyesema watu weusi vituko...kanimaliza.....kweli sis mwisho......

    ReplyDelete
  5. sasa wewe unasema eti tuige mfano wa huyu mama, yaani badala ya kuwasafirisha kuku kwenye tenga eti tuwabebe mgongoni, hata enzi ya kuwabeba watoto migongoni ilishapitwa na wakati eti wewe bado unaongelea kuku, haki za binadamu bado ni ndoto kwa nchi nyingi duniani ati wewe bado unaongelea haki za kuku ahahahaaa!!!

    ReplyDelete
  6. Unaweza kabisa kumuona huyo Jogoo amepitiwa na Ka-Usingizi kidogo kwa Raha ya kubebwa. Bi Mkubwa Hongera.

    ReplyDelete
  7. Wewe unaongelea haki za wanyama, huyu mama hajui hata haki yake ni nini. Hapo amerahisisha tu kwa ajili tayari mkononi ameshikilia hicho chungu. Huyu kuku amechinjwa baada ya masaa kadhaa kwa hiyo mada yako ya haki za wanyama hapa si kweli.

    ReplyDelete
  8. Hayo macho yako! Sio jogoo huyo, angalia vizuri. Huko ndo kwa wachuna ngozi, kama hujui!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...