Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowassa akiwa pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. John Komba na wengineo wakitest ubora wa Studio hiyo kwa kusikiliza baadhi nyimbo kadhaa zilizorekodiwa na studio hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni nyumbani kwakwe Flora Mbasha (mwenye gauni damu ya mzee) huko Tabata Kisukulu jijni Dar wikiendi hii
Baadhi ya vyombo vya studio hiyo ya Msanii Flora Mbasha vikiwa tayari vimefungwa. Studio hiyo itatumika kurekodi nyimbo za muziki wa Injili na hata kuwasaidia wasanii wachanga wenye vipaji kwa ajili ya kuviendeleza. Flora Mbasha anakuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike wa nyimbo za Injili kufungua studio yake mwenyewe
Hongera sana Frola Mbasha kwa hatua mliyofikia kutufungulia Studio mpya halafu tena ya nyimbo za Injili. Tunaomba mtusaidie basi kuweka hadharani mawasiliano yenu ya simu au hata email zenu ili iwe rahisi kuwafikia kwa tunaotegemea kurekodi na kufanya booking kwenu, utaaratibu unakaeje? Sisi Waimbaji: "MAPACHA WA YESU"tunawatakia baraka nyingi za Bwana kwa ajili ya Studio hiyo mpya.Jina la Bwana libarikiwee!
ReplyDeleteHongera sana kwa hatua hii kubwa mliyoifikia katika kumtumikia Mungu. Mungu awabariki na awazidishie
ReplyDelete