Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowassa akiwa pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. John Komba na wengineo wakitest ubora wa Studio hiyo kwa kusikiliza baadhi nyimbo kadhaa zilizorekodiwa na studio hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni nyumbani kwakwe Flora Mbasha (mwenye gauni damu ya mzee) huko Tabata Kisukulu jijni Dar wikiendi hii

Baadhi ya vyombo vya studio hiyo ya Msanii Flora Mbasha vikiwa tayari vimefungwa. Studio hiyo itatumika kurekodi nyimbo za muziki wa Injili na hata kuwasaidia wasanii wachanga wenye vipaji kwa ajili ya kuviendeleza. Flora Mbasha anakuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike wa nyimbo za Injili kufungua studio yake mwenyewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Frola Mbasha kwa hatua mliyofikia kutufungulia Studio mpya halafu tena ya nyimbo za Injili. Tunaomba mtusaidie basi kuweka hadharani mawasiliano yenu ya simu au hata email zenu ili iwe rahisi kuwafikia kwa tunaotegemea kurekodi na kufanya booking kwenu, utaaratibu unakaeje? Sisi Waimbaji: "MAPACHA WA YESU"tunawatakia baraka nyingi za Bwana kwa ajili ya Studio hiyo mpya.Jina la Bwana libarikiwee!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kwa hatua hii kubwa mliyoifikia katika kumtumikia Mungu. Mungu awabariki na awazidishie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...