Mtoto Lemmysa Bahati Singh akiwa tayari ametimiza miezi minne tangu kuzaliwa kwake.
Familia ya Meneja Matukio wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bahati Singh pamoja na mkewe Zeenat Singh,leo ambapo Ulimwenguni wanasherehekea siku ya Valentine,wao wanasherehekea zote mbili,Mosi wanatimiza mwaka mmoja wa ndoa yao,na pia siku ya Valentine,kama vile haitoshi wanamshukuru Mungu kwa kuwapatia mtoto wa kike aitwaye Lemmysa akiwa ametimiza miezi minne mpaka sasa. Kila lakheri na mafanikio mema kwa Familia ya Bahati Singh,Kikubwa ni kumtanguliza Mungu kwa kila jambo,upendo,uvumilivu vitawale kwenye ndoa yenu na pia kuwatakia maisha marefu daima-Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mwaka tu sherehe, mtasherehekea kila mwaka? Kazi kweli kweli. Kinachosherehekewa kwenye ndoa ni jinsi gani mmeweza kuvumiliana na kuendelea kupendana kwa muda mrefu at leat 10 years, but normally 25, 50 and 75. Hizo sherehe za miaka midogo midogo fanyeni privately watawacheka watu mtakapoachana japo hatuwaombei.

    ReplyDelete
  2. This is ridiculous bwana we are not interested with this stupid individual news

    ReplyDelete
  3. Waacheni wajipongeze kunawengine hata wiki hawamalizi na ni hapo hapo bongo na wengine hawaja jaliwa watoto, acheni hizo hongereni singh na mkeo.

    ReplyDelete
  4. michuzi wengine wakiwekewa comment 'mbaya' unaminya lakini hiyo ya pili umeona sawa ehe? kusema kweli hongereni, kuna nyingine mwaka hazifiki kila mmoja na lwake. na wanasema hakuna kipindi kigumu katika maisha ya mke na mume kama mwaka wa kwanza.

    ReplyDelete
  5. Wachangiaji wa kwanza na wa pili, kama nyinyi hamko interested na hizi news basi msiisome. Full stop. Hongera Bahati, Zeenat na mtoto wenu na tunamwomba Mwenyezi Mungu awalinde na awape kila la heri. Amin. Julius.

    ReplyDelete
  6. sasa hawa ni mabaniani? au masingasinga?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...