Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Mohamed Rashid Mkaazi wa Majohe mmoja kati ya majeruhi walioathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea juzi usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika kambi ya JWTZ Gongolamboto jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili leo, kwa ajili ya kuwafariji majeruhi hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwafariji majeruhi mbalimbali waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu kutokana na kuathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea juzi usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika kambi ya JWTZ Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Devis Gwaga (15) mwanafunzi wa kidatu cha 3 katika shule ya Sekondari Ilala, mkaazi wa Majohe aliyelazwa katika Hospitali ya Temeke kwa matibabu ambae ameumia miguu kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea juzi usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika kambi ya JWTZ Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Anjelina Magoma Mkaazi wa Majohe aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu ya miguu kutokana na kuumia vibaya na milipuko ya mabomu iliyotokea juzi usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika kambi ya JWTZ Gongo la mboto jijini Dar es salaam.Picha na Amour Nassor VPO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mimi Kila nikiona hizi picha natamani nisirudi tena kwenye blog, maana nikiweka maoni yangu halisi na mtazamp wangu hayatolewi.

    ReplyDelete
  2. karne ya 21 wagonjwa wanalala chini jamani?daa inatia huruma sana africa sijui tutafika lini saa nyingine nahisi kama tumerogwa!!

    ReplyDelete
  3. Kwakweli yasikitisha sana,wagonjwa kulazwa chini kiasi hiki!!!? Hivi viongozi wetu hawajisikii aibu,na kuhisi ya kwamba ipo siku wataulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu juu ya laia wao?Kabla ya wabongo na sie kuanza kuandamana ... Kuna haja gani ya kutemberea magali ya kifakhari mishahara mikubwa hali ya kuwa nyanja nyingi hatuja jitosheleza ikiwemo upande wa afya??? Twawapa pole wale wote walio athirika na mabomu ya Gongo lamboto.

    ReplyDelete
  4. Hii haitakua mara ya mwisho kwa vile mara ya kwanza wahusika hawakuwajibishwa kisawa sawa sasa ni nini kitazuia tena mara nyingine...Nobody cares as long they still have a J.O.B

    Oh well just poor people keep dying in vain...

    ReplyDelete
  5. Haya maghala yangehamishiwa Oyster Bay, Masaki na Mbezi tungeona kama yanalipuka hovyo hovyo hivyo..

    ReplyDelete
  6. makamu wa rais swali hili ni lako,JWTZ,JKT,haya ni majeshi ya nini hapo tanzania?usije mikono nyuma hapo kwa kuondoa ngoma juani hapo hospitali,kunakufa kijinga sababu ni nyinyi

    ReplyDelete
  7. Tanzania nakupenda mmmmmh mmmmh! mafisadi jamani sisi wa kipato cha chini tunatia huruma jamani mmh mmh.Yaani jinsi gani tunavyoonekana wajinga na mbumbumbu. Hii issue imetokea walipost kwenye yahoo home page mariporter waliwasiliana na viongozi wahusika wakasema no comment. na wenzetu wanatushangaa jinsi gani tulivyo wapupavu na kama tuna mtindio wa ubongo. Watawekaje base kwenye makazi ya watu mji umepanuka jamani inasikitisha sana. Ila sishangai juzi nilienda kumuinterview export meneja wa kampuni fulani akasema anaifahamu tanzania vizuri sana iko very corruption eti anafanya dili hajui kuwa huku wanakuwa monitor. Je, tutafika jamani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...