Habari za siku nyingi Ankal!

Nimepata hii toka Mtoni Kijichi wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam maeneo ya kota za Benki na Polisi karibu na Kijichi Sekondari. Sijui kama Magufuli anajua kuwa pamoja na juhudi za manispaa ya Temeke kupafanya pawe tambarare, kuna jamaa wanaona kuwa nyumba zao ni muhimu zaidi kuliko huduma ya barabara. na wanasema hawababaishwi na mtu na hakuna wa kuwafanya lolote.... Tehe tehe teheeeKaaazi kweli kweli. Magufuli na Mwakyembe mmeona mambo hayo???

Mdau Mtoni kijichi

fanya fyoko uone...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mangi wa KiboshoFebruary 10, 2011

    Mbagalaaa! mbagalaa! tatizo kwetu mbagalaaaah hapo nyuma mbele jalalaaah! tatizo kwetu mbagalaaaah!!!! hahahaaaaaaaaaaa! Mbagala ya Wamakonde,wazaramo na Waganga wooote wa kienyeji wanakaa Maeneo haya

    ReplyDelete
  2. Duuu!!! hii nayo ni kali ya 2011, au kulikuwa na waigizaji walikuwa wana-act hapo? maana haiingii akilini vizuri.

    ReplyDelete
  3. tatizo kwetu kimara majambazi kila siku wanatuua

    ReplyDelete
  4. Hii mbona haijakaa sawa,sasa hao waliofunga njia wanapita wapi?inanikumbusha sinema molja ya kihindi Mwamba mmoja alizuia kibabe watu wasichote maji,Mithun Chakrabot akaja kumdunda

    ReplyDelete
  5. Hakuna sehemu nzuri ya kuishi kama Mbagala,kila kitu kipo na bei chee, yale mabomu ndo yalitia watu hofu,lakini baada ya Raisi kutangaza kuwa hakuna tatizo kama hilo tena kila mtu anaishi kwa amani,ule ulikuwa mziki tu ambao umewakilisha jinsi Tanzania isivyojali usafi wa mazingira,kila kona ya mji hata katikati ya mji utakuta vifurushi vya takataka. Ila ukitaka kuishi Mbagala uwe ndani ya geti ili usiombwe chumvi kila saa. Huyo aliyeweka visiki barabarani atakuwa anasababu yake ya msingi kama sio kichaa.

    ReplyDelete
  6. DuhHata mi sielewi.... huko hakuna sirikali za mtaa wala mwenyekiti ama balozi ambao nadhani wapo pamoja na misele mingine wanatetea na kulinda haki za msingi za raia kama vile kuwa na barabara walao inayoeleweka na kupitika hata kama kwa ze bajaji!!Huyo aliyeweka visiki ni gaidi na lazma aondolewe ama yeye ama visiki vyake maramoja..... halafu hili pia mnalipeleka kwa Dk Magufuli..... wananji wa hapo hawaoni misri wanafanza vip.... kudai.....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...