Mange Kimambi

Kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya watanzania mtandaoni,bila shaka utakubaliana nasi kwamba miongoni mwa mahali ambapo mengi hutokea na mengi huandikwa kama sio kujadiliwa basi mahali hapo ni katika blog inayokwenda kwa jina la U-turn.

Ni blog ambayo ingawa haina umri mkubwa(ilianzishwa mwaka mmoja na nusu tu uliopita), tayari imefanikiwa kuwa chanzo muhimu cha habari,michapo,maoni,matukio bila kusahau udaku wa hapa na pale.Ni mafanikio ambayo sio ya kubeza.It is what it is!

Mwendeshaji na mmiliki wa U-turn si mwingine bali ni Mange Kimambi ambaye miaka michache iliyopita ilikuwa ukisikia jina lake basi ilikuwa ni kupitia kurasa mbalimbali za magazeti hususani yale yanayoitwa “magazeti pendwa”. Leo hii mambo ni tofauti. Ni mama,mke,mwanafunzi na blogger mwenye idadi kubwa tu ya wasomaji na wafuatiliaji.

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya kina. Hii ni mara ya kwanza kwa Mange kufanya mahojiano ya kina na chombo chochote cha habari.

Je,Mange ni nani hasa?Ametokea wapi mpaka kufikia alipo hivi sasa ambapo kila siku idadi ya wasomaji na wanaofuatilia maisha yake na anachokiandika inazidi kuongezeka? Ni matukio gani katika maisha yake ambayo kwa namna moja au nyingine yamechangia in making her who she is today?

Nini siri ya mafanikio yake au ya blog yake?Unataka kujua ana maoni gani kuhusu mambo mbalimbali kama vile uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?Ana ushauri gani kwa wasichana wadogo(teen girls)?

Kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi,
fuatana na blogu dada ya Globu ya Jamii iitwayo BongoCelebrity katika mahojiano yafuatayo:
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hey Mange, I'm kinda of coy to say whole lot of stuff but since that you're here as a public figure then lemme give you something. Nimesoma interview yako na iko pretty good but nina swali na maoni if you don't mind and here we go...Maisha uliyoishi si mageni kwenye jamii yetu,me personally I was brought na mama wa kambo so the song you singing is very known to me now, kitu cha msingi kwako as I did you need to learn how to forgive and honestly I can understand what is eating you and apparently is grief and anger. For you to move forward first you need to forgive your step mother and two you need some grief pros to walk through your dad's loss and I'm sure that you're a smart person and resiliant to bounce back.
    Kitu cha mwisho kwako mange, since that umeona mambo ya mama wa kambo yalivyo complex then nakushauri umchukue binti yako bokhe um raise ili isitokee what happened to you and make her blame you for being raised na watu wengine maana naona baba ake yuko busy muda wote na ma party ya ice black.
    Thank you so much

    ReplyDelete
  2. mange hata mimi nakushauri umchukue mtoto wako bhoke umlee mwenyewe, kwa jinsi baba yake alivyo hayuko kimalezi sana, japo anaishi nchi zenye sheria kali juu ya watoto lakini ujue mtoto wako akikua hatakuwa proud of you..ila ni mama yake wa kambo kama ilivyo kwako unamtaja mama wa kambo zaidi kuliko mama mzazi....sasa na bhoke kama atapewa malezi mazuri bila kuteswa na huyo step mother wake basi atamtaja huyo mama kuliko wewe...MANGE WANAWAKE WENGI HUPIGIANIA KULEA WATOTO WAO HASA WASICHANA WA SASA HIVI KWANINI WEWE USIMCHUKUE MWANAO?...

    ReplyDelete
  3. Na mimi naunga mkono kabisa, kwani yeye mange pia si mtu wa maparty mtoto atalea saa ngapi? uoni mpka kaweka housegirl? sisi ulaya watoto tunalea wenyewe na tunapokelezana kama mr anatoka na friend zake ama mimi...sasa mange hawezi kashazoe mashauzi ulezi ¨kazi..mtoto wangu nitalea mwenyewe maishani kwangu labda niwe mgonjwa..lakini sio kwa kula good time..childhood haiji mara mbili..huu ndio wakati wa bhoke ajuane na mdogo wake wakue wote kwani dubai hakuna international school??? dada mange kachemsha eti mama wa kambo..yeye ndio alikuwa anamuonea wivu mamayake wa kambo kwa baba yake

    ReplyDelete
  4. Huyu mama u celebrity wake ni kutangaza mambo yake ya familia tu kwenye website yake. Hakuna chochote zaidi alichofanya kwenye jamii cha kumfanya awe mfano kwa watanzania au celebrity. Ni yeye tu anayeendesha web site ambayo wehemu kubwa ni majadiliano kuhusu maisha yake, mumewe na watoto wake. Huu ni mtazamo wangu lakini kwa vile natofautiana kidogo na wengine nitaitwa "hater" na nii post haitatoka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...