Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo (pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei, Naibu Gavana B.Juma Reli (kushoto) na mwakilishi wa MasterCard Bw. Daniel Monehin (Kulia) wakionyesha mfano wa kadi ya TemboCardMasterCard iliyozinduliwa rasmi na Benki ya CRDB katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya MovenPick jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Charles Kimei akimkabidhi Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo kadi ya kwanza ya TemboCardMasterCard. Kushoto ni mwakilishi wa MasterCard Bw. Daniel Monehin.
Moshi, nderemo na vifijo vikiashiria kizinduliwa rasmi kwa TemboCardMasterCard ya benki ya CRDB.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo akihutubia hadhira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo
Viongozi wa serikali, Benki ya CRDB na MasterCard International wakishuhudia uzinduzi rasmi wa TemboCardMasterCard
THT wakiburudisha hadhira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kulekule kwa chinova TEMBOCARDMASTERCARD ndo yale aliyokuwa anayasema Dr. Mwakyembe why not Tembo Master Card!!!

    ReplyDelete
  2. MsemaKweliMarch 21, 2011

    Jamani hizo tembo card lakini mashine za ku-process hizo card madukani au kwenye POS(place-of-sale) yeyote zipo wapi? Hii haisaidii kwa sababu utaenda dukani hawapokei hiyo tembo kadi yako. Yaani kadi zinatumika kutolea hela kwenye ATM tuu. Wadau na wajasilimali credit cards processing companies zinatakiwa sana bongo. Angalai nchi kama Kenya au South Africa zimetupiga bao kibao kwa hili jambo. Tuache na kubeba magunia ya noti kwenda dukani.

    ReplyDelete
  3. Ningependa kujua kama kadi hizi ni sawa kabisa na kadi za ughaibuni, ambazo zinamwezesha mtumiaji kulipia huduma mtandaoni au kununulia vitu mtandaoni, kwa mfano vitabu.

    ReplyDelete
  4. TemboCardMasterCard MY FOOT! Why this now?! Tembo Master Card would have been better....

    ReplyDelete
  5. Mbele,
    nilihudhuria hiyo function, kwa maelezo marefu yaliyotolewa inaonekana ni sawa kabisa na hizo za ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...