Sheria za kupata viza za wanafunzi nchini Uingereza zinatarajiwa kuwa ngumu zaidi- baada ya kuibuka wasiwasi kuwa mbinu za kuingia nchini humo kwa minajil hiyo hutumiwa kiudanganyifu

Waziri wa mambo ya ndani Theresa May alisema viza za wanafunzi hazitumiwi inavyotakiwa na "wengi wamekuja hapa kufanya kazi na si kusoma".

Alitangaza mpango wa kupunguza idadi ya viza za wanafunzi kufikia 80,000- takriban robo ya idadi iliyopo sasa.

Waziri kivuli wa wizara ya mambo ya ndani Yvette Cooper alionya sheria hazitakiwi kuharibu idara zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni tano kwa mwaka.

Bi May aliliambia bunge kuwa matumizi mabaya ya viza za wanafunzi yamekuwa "ishara ya mfumo wa uhamiaji uliotumiwa vibaya".

Nenda BBC Swahili kupata habari kamili.

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jamani achaneni na uingereza. Its no longer a big deal kupiga shule au kazi huko. Kuna maeneo kibao sasa. Korea, Malaysia, Japan, Ujerumani, nknk...
    Hao jamaa wameshafunga hata Ubalozi hapa Dar es Salaam. You dont have to admire UK anymore,

    ReplyDelete
  2. wamefilisika na sera hawa jamaa. sera za kiubaguzi zimepitwa na wakati. Ni kweli sasa hivi kuna vyuoo vizuri kutoka far east.

    ReplyDelete
  3. Tena Malaysia ni rahisi, walimu wanasomesha vizuri, hali ya hewa kama bongo tu. Uingereza unabaguliwa na kila mtu, kuku, mbwa hata ukimaliza akili imeshapungua.

    ReplyDelete
  4. NI KWELI KABISA WADAU KWANI TUULIZENI TULIOKO HUKU NDO HALI TUNAIJUA JINSI ILIVYO TUNACHAKACHULIWA SANA KAMA MAHOSPITALINI HUKO UTAKUTANA NA MGONJWA ANAKWAMBIA HATAKI KUHUDUMIWA NA MTU MWEUSI UNATUKANNWA... LAKINI NDO HIYO TUNAENDA NA STAILI YA,,, KAMATA MWIZI MEEN,, YANI KIUBISHI UBISHI..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...