Vuguvugu la kudai katiba mpya linazidi kupamba moto sasa Tanzania, kila Sehemu watu wanadai katiba mpya, tayari chama cha wananchi CUF kimefanya maandamano yaliyoongozwa na kaimu katibu mkuu Julius Mtatiro lengo kuu la maandamano hayo ni kuitaka serikali kuridhia kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati huohuo chama cha wafanyakazi Tanzania maarufu kama TUCTA kupitia kwa katibu mkuu wake Nicholas Mgaya tayari kimeshatangaza kuwa swala la mabadiliko la katiba ni la lazima na kwa upande wa CHADEMA tayari na wao wameshatangaza kupitia kaimu katibu mkuu wake John Mnyika kuwa ni lazima serikali ikubali kubadili katiba pia hali ipo hivyohivyo kwa viongozi wa dini nchini ambao kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakisema kwa msisitizo kuwa katiba tuliyonayo imepitwa na wakati ni muhimu kwa serikali kuridhia mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.
Endelea kusoma
KWA KUBOFYA HAPA
Endelea kusoma
KWA KUBOFYA HAPA
Hivi hawakusikia kuwa serikali imeridhia hilo, Toka mwaka jana? Hizo ni njama tu za kutudivert na mambo muhimu, lete habari za Loliondo Ankal! Watu wana hamu na ze Kikombe's
ReplyDelete