Leo ikiwa ni takriban siku kumi tangu Dada Mage aaanze kutibu wagonjwa kwa tiba anayodai kuwa kapewa na uwezo huo na Mwenyezi Mungu, Mtaa huo wa Urban Quarter umeanza kuwa maarufu hasa baada ya wachuuzi wa vyakula vya kila aina kuanza kutoa huduma hapo. Kama uonavyo leo pana takriban watu 2000 hivi ukifananisha na jana ambapo palikuwa 500 hivi. Kwa picha na habari zaidi mtembelee Mkala Fundikira katika keronyingi blog.
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwananch gazeti lao hawataki weke habari za huyu dada wao kila siku babu wanaona ataharibu biashara au watu watashtukia

    ReplyDelete
  2. Ujinga na elimu duni umewatawala baadhi ya watanzania,na kuwa na imani ndogo ya kumuamini Mnyeezi Mungu, na ndiyo maana ni rahisi kuwadanganywa!

    ReplyDelete
  3. Simwamini kabisa!!! Utapeli umeanza!

    ReplyDelete
  4. Hivi hawa wote hakuna anayefanya kazi kabisa? Huu muda watu wanautoa wapi? Watu wamrudie Mungu magonjwa yatapungua maana naona kila mtu mgonjwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Jamani! acheni kutia mchanga katika kitumbua cha mwenzenu. Watu wanafanya kila njia kutafuta pesa...wizi, kuua walemavu wa ngozi, kutapeli, kuuana, nk. Hii ni namna tu ya ujasiliamali msishangae.

    Somo:
    Kama huna imani na mwenyezi Mungu mmoja(Muumba wa kila kitu) na hujauelewa ujumbe ulioletwa na wajumbe wake kwetu sisi viumbe ni rahisi sana kukumbwa na hii imani potofu " ya kuamini kikombe kinaponya"

    Mungu atusamehe na kutuongoza
    Amini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...