Leo ikiwa ni takriban siku kumi tangu Dada Mage aaanze kutibu wagonjwa kwa tiba anayodai kuwa kapewa na uwezo huo na Mwenyezi Mungu, Mtaa huo wa Urban Quarter umeanza kuwa maarufu hasa baada ya wachuuzi wa vyakula vya kila aina kuanza kutoa huduma hapo. Kama uonavyo leo pana takriban watu 2000 hivi ukifananisha na jana ambapo palikuwa 500 hivi. Kwa picha na habari zaidi mtembelee Mkala Fundikira katika keronyingi blog.BOFYA HAPA


Mwananch gazeti lao hawataki weke habari za huyu dada wao kila siku babu wanaona ataharibu biashara au watu watashtukia
ReplyDeleteUjinga na elimu duni umewatawala baadhi ya watanzania,na kuwa na imani ndogo ya kumuamini Mnyeezi Mungu, na ndiyo maana ni rahisi kuwadanganywa!
ReplyDeleteSimwamini kabisa!!! Utapeli umeanza!
ReplyDeleteHivi hawa wote hakuna anayefanya kazi kabisa? Huu muda watu wanautoa wapi? Watu wamrudie Mungu magonjwa yatapungua maana naona kila mtu mgonjwa sasa.
ReplyDeleteJamani! acheni kutia mchanga katika kitumbua cha mwenzenu. Watu wanafanya kila njia kutafuta pesa...wizi, kuua walemavu wa ngozi, kutapeli, kuuana, nk. Hii ni namna tu ya ujasiliamali msishangae.
ReplyDeleteSomo:
Kama huna imani na mwenyezi Mungu mmoja(Muumba wa kila kitu) na hujauelewa ujumbe ulioletwa na wajumbe wake kwetu sisi viumbe ni rahisi sana kukumbwa na hii imani potofu " ya kuamini kikombe kinaponya"
Mungu atusamehe na kutuongoza
Amini