Visit Babu at Samunge

with Kibo Travel Bureau For booking: 0767476424 Day – 1: Dar es Salaam – Arusha (647km)

Early morning we will begin our journey.

A day driving to Arusha by luxury bus Overnight: HB. Hotel Mc-Ellys Arusha (or similar) http://www.mc-ellyshotel.com/index.html Day – 2: Arusha – Mto wa Mbu - Samunge (Loliondo) (about 400km) After breakfast, we will meet our safari vehicles 4x4 and begin a long driving day to meet the stretched queue to Samunge village where Babu is. Overnight: FB. In A modern dome tent near the car, each tent will be used by 2-3 participants.

For full information CLICK HERE.

Mchungaji Ambilikile akiendelea kumwaga dozi huko Loliondo Watalii toka nje ya nchi wakishukuru kwa kupata kikombe

Mama akimpatia mwanae kikombe foleni bado ndefu
Mtalii kapiga kambi, wenzie wako kwenye foleni
Foleni wakati kinachomoza leo
Huko bila four wheel drive usipeleke mkoko




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Michuzi naomba tuwajadili wa Kenya (Neighbors from Hell) yaana Majirani kutoka kuzimu. jinsi wanavyo tuchukia Watanzania na kufanya hila ili tuwe chini wao waende Juu.

    Wameandaa Makala ya Kupinga Tiba hii (Loliondo Wonder). Wakati walikuwa wanadanganya dunia mlima kilimanjaro uko kwao.

    2. Wametuibia Tanzanite na wao ndiyo wanaongoza kuisafirisha nje.
    3. Wanajenga uwanja wa ndege karibu na mpakani moshi ili watuibie watalii wasije kutua KIA.
    4. Wanapinga hii Tiba kwa wivu ili kuzuia wakenya wasije na kuzuia umaarufu wa Tanzania.
    5. Walikuwa wanapinga zile pembe za ndovu zilizokuwa za maharamia zisiuzwe kunufaisha nchi yetu na wakashinikiza zichomwe moto.
    6.Wanazuia tusijenge barabara ya serengeti ili tusinufaike.
    5..Hawa kweli ni Majirani kutoka Kuzimu (Neighbors from Hell).

    Hebu tuwajadili
    Mdau Dar es salaam.

    ReplyDelete
  2. In his Sermon on the mount, Nabii Isa bin Maryam RAA said
    But I tell you who hear me:
    Love your enemies,do good to those who hate you
    Bless those who curse you
    Pray for those who mistreat you. If someone strikes you on one cheek, turn to him the other also. If someone take your cloak, do not stop him from taking your tunic.
    Give to everyone who asks you,and if anyone takes what belongs to you,do not demand it back.Do to others as you would have them do to you
    Luke 6:27-31 NIV
    That is for anonymusSun02.47
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. Hivi Mnamkumbuka ankal Kamau alivyotutukana matusi makubwa kisa ujio wa Timu ya Taifa ya Brazili? Kila mkitaka kupata kitu kizuri huwa anazuka mkenya fulani na kuchafua hali ya hewa. WIVU WIVU Sasa huu ni ujirani gani?

    ReplyDelete
  4. We wakatabahu unaishi dunia ipi? yaani jamaa wakija kukuomba wewe utagawa tu?na wakikuchapa upande mmoja utawapa na wachape upande wa pili?na jamaa wakichukuwa vitu vyako wala hautawaambia warudishe kama wanabana navyo?

    Lakini uwongo mbaya na kiswahili ni kirefu, jamani hamna mtu hata mmoja aliyepima baada ya kutoka loliondo?hata kama ingekuwa ni asilimia 5 tu wamepona, imagine upunguze ukimwi Tanzania kwa asilimia tano, si ingekuwa ni mafanikio makubwa sana tu?

    Natoa wito na changamoto kwa watanzania, wakapime, kama wanao waende kwa babu, wakirudi wakapime tena, baada ya hapo tuamue cha kufanya, maana hapa sioni yanini malumbano...

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa kwanza,
    wewe una wivu,choyo na Fitina kama watanzania wengine,
    1.Tiba ya Babu haina majibu ya utafiti wa kina wa kikemikali.kwa upeo wako tu wakawaida,kikombe kimoja kitawezaje kupona magonjwa chungu mzima,bila kujali ujazo,uzito au umri wa mtu n.k
    serekeli inashindwa kufahamu ewapo hayo maji yatakua na sumu na kuwa na madhara makubwa mbele ni watu wangapi wata dhurika.Viongozi wetu uuzo nao kwa hofu waliyonayo ya kutokana na maradhi sugu yanayo wasumbua wanakimbilia na kuwa mfano pumbafu wa hili swala,
    jamani mambo mengine yanalitia taifa letu ujinga.
    2.WEWE NI MJINGA:
    3.sasa kwanini serekali yetu haijengi viwanja vingi vya ndege?pesa haina?wafadhili?
    4.Anamawazo duni na yakimasikini sana,
    5.jamani tupelekeni watoto shule,
    6. Bara bara isijengwe serengeti auhifadhi yeyoyte kwa sabababu chache zikiwemo (a) zitapoteza uhalisia.
    (b) zitaongeza msongamano wa watu kwenywe hifadhi na ku - disturb Eco system .
    (c) kama zikianza kujenga bara bara mtawaza na hoteli lounge n.k
    tuta viingilie na kupoteza haki ya vile viumbe vinavyo hshi hapo kwa karne nyingi kwa kujali tu manu faa yetu.
    7.kijana hii mipaka waliweka tu wakoloni ili kuweza kuzigawanya mali na urithi wetu wapekee tuliojaliwa,
    tazama ramani yako vizuri,hiyo mistari isiweke tofauti au pingamizi ya kutumia faidi ya urithi wetu.
    8.Nenda shule
    Arica Unite
    Dr M. Heinz
    Vienna
    .

    ReplyDelete
  6. ujinga na umasikini vinashirikiana hapo kuitafuna nchi ya waswahili.

    ReplyDelete
  7. Habari ndungu zangu wa Tanzania.
    Acha nichangie mada ya ndugu hapo juu kuhusu wakenya.
    Mimi binaf siwapendi wakenya,Wanajifanya wajuaaji sana.Mimi naishi Usa hapa kunawakenya kibao,Wazungu pia si watu wazuri sana,Lakini nikiambiwa nimchague mkenya na mzungu nitamchagua mzungu.kwani angalau hawa wanamoyo wa kibinadam kidogo si sawa na wakenya,

    Sasa turudi kwa babu loliondo.Jamani jamani nasikia huruma kidogo kwa Babu na watanzania wanao pata tiba kwa babu.hao wazungu mnao waona hapo hawakwenda kwa babu kupata dawa kama mnavo dhania wana lao hao.Mda si mrefu mtasikia dawa haifanyi kazi tena ama ita lolote laweza tokea.Wanalo hapo wataharibu kila kitu hapo mwisho wa siku mtasikia dawa haifanyi kazi ama mkapata madhara yoyote kwa watumiaji.

    Kwa nini nasema hivi kwa uchungunz wangu mdogo,Hawa wazungu wanaingiza pesa kwa kutuuzia dawa wa bongo na dunia nzima ote.Mfano mzuri asilinia 95 ya watu waishio usa wanatumia dawa kwa sababu tofati tofauti.
    1 nyakula nya hapa vimeweka madawa ya kukuharibu mwili wako.
    2Maji ya hapa ameweka dawa ambazo si sawa kwa mwili wako.
    3na sasa nyakula hivi vimeenea bongo pia.
    wenyewe mnaita mambo ya kisasa,lakini si ya kisasa yanatuua,
    mfano kama hawa kuku wa kizungu si wazuri kwa afiya yako,
    ngombe wa kisasa si wazuri pia,nyakula nya makopo na kadhalika si vizuri.
    Lakini kwa kua msikini weee WATZ tulio wengi hatuma elim ya kutosha tunakula tu,mwisho wa siku na sisi bongo tutanza kuishi kwa kutumia dawa.

    Sasa ndio maana na sema hivi hao watalii mlio waona hapo.Hawapo hapo kwa kheri,kama si hawa basi kunawengine wapo jian wanakuja.kwani babu anaharibu bishara ya hawa jamaa,Jamani kama hamuamni tusubiria na tuone mwisho wa babu.

    Asanteni
    Mdau Usa

    ReplyDelete
  8. Tatizo tusiwe watu wa kulalama lalama tu.
    Sisi wenyewe ndio wazembe na tumelala ndio maana wenzetu wanachukua hiyo advantage.
    Wewe fikiria hatuna hata ndege Air Tanzania iko wapi leo? Halafu tunategemea watalii waje kwetu?
    Viwanja vya ndege vyenyewe duni, ndo maana wenzetu wajanja wanajenga jirani tu.
    Tumezubaa sana wabongo yaani tumelala inabidi tuamke, na tushachelewa sana. Ndo maana tunahitaji viongozi wazalendo, wenye uchungu wa nchi, wasio wabinafsi, wanaoangalia maslahi ya Taifa, wasio mafisadi. La sivyo tutakuwa tuna-dream to daima.
    Na pia madau aliyesema tusamehe, ni sawa lakini si katika mambo kama haya, huo utakuwa ni ujinga. Tunatakiwa kusimamia, kutetea, na kupiginia nchi yetu. Tuangalie nchi zilizoendelea tujifunze. Tuachane na haya mambo eti, Akikupiga kofi shavu la kulia mgeuzie na la pili. Nchi haiwezi kwenda kwa namna hiyo hata kidogo!

    ReplyDelete
  9. Hawa wakenya ni wajinga sana. Ona wanavyotoa comments na kiswahili chao kibove halafu wanajidai watanzania. Hawa waogopeni kuliko mnovyoogopa ukimwi. Ni mafisi wakubwa wasio na hata chembe ya utu. Mkiwaendekeza mtaona ya firauni. Nyerere aliwaita manyang'au hakukosea.

    ReplyDelete
  10. wakenya wataendelea kuwa juu na sisi wadanganyika tutaendelea kudanganyika yote hayo kutokana na elimu mbovu tuliyonayo viongozi wenye roho mbaya na kujali maisha yao binafsi nchi inadidimia wenzetu wakenya kila siku wanabuni jambo jipya la kupata maendeleo wakati wadanganyika ndio kwanza wanaimarisha rushwa

    pale uwanja wa ndege wa dar es salaam ukifika na mzigo wako huko ulipotoka umenunua huo mzigo kiasi cha dolla 200 ukifika pale wanakuchaji ushuru laki tatu 3 yani ushuru unakaribia bei uliyonunulia huo mzigo

    sasa basi kutokana na bei ya ushuru kuwa juu inabidi upatane na wahusika na kuwaomba wakupunguzie matokeo yake wanakupunguzia kutoka laki 3 mpaka laki 1 na unapolipa laki 1 ina maana hiyo ni kinyume na mipango ya kodi ya serikali kwahivyo huwezi kupewa lisiti ya malipo

    hiyo laki 1 inaingia mfukoni kwa huyo mhusika hapo kazini hapo tayari rushwa imepewa nafasi kubwa sana
    sababu ya kuijenga rushwa ni kuweka kodi kubwa sana kiasi mtu anashindwa kulipia na matokeo yake anaona bora alipie kidogo kwa njia ya rushwa

    je serikali inafaidika nini kwenye hiyo kodi?
    je serikali ingeweka kodi kiasi cha hiyo rushwa mfano laki 1 hapo sioni kama mtu angetaka kutoa rushwa sababu uwezo wake ungemuwezesha kulipia huo mzigo kwa laki 1 na angepatiwa lisiti na serikali ingenufaika

    matokeo yake mtu analipia mzigo kwa laki 1 na serikali haijapata chochote

    ushauri wa bure kwa wahusika wa kodi za serikali wekeni kodi zinazofanana na biashara au mzigo unaohitajika kulipiwa kodi msiweke tu kodi ambayo itamfanya mtu ashindwe kulipia na matokeo yake atatoa rushwa ili aokoe mzigo wake usibakie pale uwanja wa ndege.

    mdau wa mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  11. Baba KidedeaMarch 28, 2011

    He he he..wa Tanzania sisi ni watu wa ajabu saaana.. Afadhali hata watani zangu wazaramo wanaishia kucheza segere.. Yaani kila siku tunalala na kuwaota Wakenya..ni lini tutasahau na kufikiri vitu vya maana.. Lazima tukubali wakenya hatuwawezi..wana damu kama ndugu zangu kina Meku..wachagga katika biashara na kuangaika.. Sisi wa Tanzania ni wavivu na tumejaa malalamishi tu..NTV wametengeneza documentary ambayo hakuna media yeyote yetu imeweza tengeneza halafu tunapiga kelele.. Tuamuke ndugu zangu Marehemu Dokta Remmy alisema..........tutaishia kuangalia mipira ya UK na kucomment pumba kwa Michuzi kila siku...Nenda Shule,..fight for your life and don't blame your neighbour for your poverty!

    ReplyDelete
  12. Acheni kujidharau tumieni takwimu mnapoongea. Nahisi hawa ni wakenya waliojifunza kiswahili kizuri ndio wanajidai watz. Mpaka sasa hivi takwimu za dunia zinaonesha wakenya wanaoishi chini ya dola 1 kwa siku ni 50% ambapo Tz ni 36%. Hapa nani maskini? GDP yao na ya kwetu hazitofautiani sana. Elimu ya Tz ni nzuri sana ila ninyi mnaojidharau ndio hamjui kuitumia elimu yenu. Na kama nyie manaoandika ni wakenya basi mjue hatutaiga elimu yenu hata siku moja na mtaona elimu yetu itakavyotupaisha. Huyu mjinga ameshasema tatizo ni viongozi wabovu halafu tena anasema elimu. Na kama mlijua viongozi ni wabovu kwanini mliwapa kura uchaguzi uliopita? Nyinyi ndo wajinga. Mliacha viongozi walioonesha nia ya kuleta mabadiliko mkachagua mafisadi. Liweni kadiri iwezekanavyo. Hao wakenya wataendelea kuwa wajinga tu na mawazo yao finyu yalojaa wivu. Watz wangapi wamesoma ulaya na marekani toka vijidudu hadi PhD lakini hamna cha maana walichofanya. Elimu ya Tz juu sana, Kagame, Museven, Jose kabila walisoma elimu ya Tz. Je hawafanyi mambo ya maana?

    ReplyDelete
  13. Kilichonishangaza ni kuwa WAKENYA wametengeneza Documentary na wameirusha tukaiona! Wako wapi ITV, TBC Myonge myongeni haki yake mpeni!

    ReplyDelete
  14. Mnaodharau elimu ya tz angalieni kina Asha rose mgiro, tibaijuka, salim ahmedi salim walivyoshika nyidhfa za kimataifa kwa msingi wa elimu ya tz. hata km walisoma nje baadhi ya digrii zao lakini msingi ni elimu ya tz. watz mna tabia ya kutojiamini na mlivyo navyo hata mkipewa elimu ya nchi gani bado mtatafuta cha kujidharaulia. Mnatumia visingizio ili mkwepe kuwajibika. Acheni huo ushamba.

    ReplyDelete
  15. Huyu Mkenya anayejiita Dr. Heinz ana tamaa sana, eti anasema tusijali mipaka ya kikoloni. Lengo lake ni kutetea kuwa mlima kilimanjaro uko kenya. Halafu anaita Mali asili za Tanzania ni "urithi wetu sote". Wanataka ardhi na mali zetu lakini hawatutakii mema. Ndio maana Wakenya hawapendi kwenda Uganda. Maana waganda hawawezi kukubali upuuzi. Tunakubali Kenya imepiga hatua kimaendelea lakini hicho siyo kigezo cha KUDHARAU NA KUENDELEA KUWATAPELI Majirani wenye nia njema na Wakenya.

    ReplyDelete
  16. Unaposema wamepiga hatua kimaendeleo unatumia vigezo gani? Mtoa maoni hapo juu amesema wakenya wanaoishi chini ya dola moja kwa siku ni 50% wakati watanzania ni 36% ambayo ni kweli. Unazuzuliwa na majengo yao? Yale sio yao ni ya wazungu waliowachukulia ardhi ndio maana sasa hivi hawana ardhi wanataka kuvamia ardhi ya Tz. Watanzania wameendelea kuliko wakenya kwani uchumi wa tz unamilikiwa na watz wenyewe kwa asilimia kubwa kuliko wakenya. Naungana na mtoa hoja anayewonya muache tabia ya kujidharau hata kwa vizuri mlivyo navyo. Hamtaendelea namna hiyo.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 08, 2011

    Hi all.Am a Kenyan who has been to Loliondo to visit Babu once.I have full confidence that Babu is send of God and i really don't care what other Kenyans are saying.I took the Medicine and am well now.Remember that those who are against Babu are those who want their status quo maintained.These are corrupt people especially Government and Non- governmental organization who are corruptly benefiting from HIV/AIDS funds and therefore do not want to imagine a cure for the same because this will render them irrelevant.
    Long live Babu , long live Tanzania.I wish you God's protection and grace.Am soon bringing another team from Kenya to visit Babu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...