Kada wa CCM, Ndg Innocent Melleck Shirima.

Habari za leo Mkubwa,

Naombeni mnifikishie ujumbe wangu huu kwa Jamii na viongozi wa UVCCM,Mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa (UVCCM) ambae hii leo nimeamua kuzungumzia hali ilivyo ndani ya umoja huo sambamba na kuweka wazi malengo yangu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa umoja huo taifa pindi muda utakapowadia.Nadiriki kusema nitafanya hivyo kwaajili ya kufanya usafi wa njia ya kuelekea Ikulu kwa mwanachama atakaeteuliwa na chama cha mapinduzi kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu.

Pili naweza sema umewadia muda kwa viongozi waliomadarakani kuachana na utaratibu wa umimi na badala yake waweke maslahi ya chama mbele kwa kuachia madaraka na kuruhusu uchaguzi huru na kupatikana kwa kiongozi mwenye haiba sahihi na alieweza kupitia angalau mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa JKT ili awe na maadili ya uzalendo sahihi.

Viongozi waliomadarakani kwa sasa wamekalia makundi na kuacha chama kikiporomoka ikiwa ni pamoja na kundi kubwa la vijana kuendelea kupoteza imani na chama kutokana na kukosa viongozi wa kuonyesha njia sahihi.

Nasema kwamba huu ni muda muafaka wa kuanza kufanya kazi ya kuandaa umoja wa vijana ulioimara wenye kutoa fursa kwa makundi mbalimbali ya vijana kuwa na sehemu ya maamuzi ndani na nje ya umoja huo.

Lakini pia kutazama kwa jicho la pili namna ya kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa vijana walio katika vyuo vya elimu ya juu na kati kwa kuwapatia mkoa maalumu wa kichama ndani ya umoja huo jambo ambalo litakwenda sambamba na ufunguaji wa matawi pembezoni na ndani ya vyuo vyote nchini Tanzania.

Uadilifu ulioasisiwa na Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere umemezwa na uroho wa madaraka unaofanywa na viongozi wa jumuiya hiyo kwani baba wa taifa angekuwa hai nafikiri asingevumilia kuona viongozi waking'ang'ania madaraka na kukaimu kwa zaidi ya miaka jambo ambalo loko nje ya taratibu na katiba ya umoja huo.

Kwa sasa kinachoendelea ndani ya umoja huo ni kujenga na kuweka vikwazo kwa kiongozi atakaeteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kuwa ngumu katika uchaguzi ujao.

Mpaka hapo naamini nitakuwa nimeeleweka vyema na kuonyesha ni namna gani viongozi waliopo madarakani wanavyotakiwa kufanya kazi yao.

Ahsanteni Sana

INNOCENT MELLECK SHIRIMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Sasa kama wewe ni kada kwani hamna sehemu yenu ya chama mkakutana na kuelezana. Au wewe chadema lakini umevaa sare za ccm?

    ReplyDelete
  2. Hamna kipya hapo!

    ReplyDelete
  3. Sijui pa kuanzia lakini ngoja niseme kwa ufupi, au wazungu wanaita "In the nut shell".... Yaani wewe unataka kuwania uongozi wa UVCCM... halafu unaanza kwa;

    A. kukosoa viongozi walioko madarakani na
    B. Kudai kuwafundisha ni jinsi gani wanavyotakiwa kufanya kazi yao

    Dah! Kila la heri ndugu yangu!!!! Ila Umemrahisishia kazi mpinzani wako maana akiichukua hii akaigeuza kichwa chini tu.... Kapita! hahahahahaaa saa nyingine mpaka najichekesha mwenyewe lol

    ReplyDelete
  4. Huyu kaka angetaka kujenga hoja angemsikiliza dogo mmoja jana usiku kwenye kipindi cha Je Tutafika Channel 10 anaitwa Sabatho ndio angepata maelezo mazuri. UVCCM kazi wanayo kama hawataachana na mfumo wa baba zao CCM baada ya miaka 5 kushne. Amkeni CCM

    ReplyDelete
  5. Alokwambia kama mafunzo ya JKT yanaleta uzalendo na uadilifu ni nani?kwani hawa wanaoshutumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma hawakwenda JKT?Tena enzi hizo JKT ilikuwa ya ukweli.Asilimia 99.5% ya wanasiasa ni wamimi,waroho wa madaraka na wapo ktk uongozi kwa manufaa yao.Angalia na ww usije kuwa kama wenzio endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo.

    ReplyDelete
  6. Rafiki yangu Meleck (Wa jina) kama umeaanza hivi kwa ajili ya kujijenga?? mmh! hapana, kwa mimi nakushauri uangalie njia mbadala usije ukaumbuka, hata hiyo bravo kwa kujtahidi kueleza hisia zako

    ReplyDelete
  7. Da huyu bwana kweli kwa kitendo hicho alichofanya cha kuwakosoa wenzie tena nje ya taratibu za kijumuia yaani vikao husika, halafu anasema anataka kuingia madarakani? inatia shaka huyu inaonyesha ni pandikizi la chadema!hata sura yake tu hajakaa ki ccm mkweli, katumwa

    ReplyDelete
  8. kama ana mawazo ya kua kiongozi wa juu basi angesubili na kutafuta oja ya msingi ili aweze kukosoa wale waliomtangulia lakini amewai kusema mapema ya bila kutoa hoja ya msingi ili linaweza kumwangusha yaani hapo amekuwa kama Placido domingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...