Mdau Kim Tenga akitafakari namna gani watafika safari yao mara baada ya ndinga yao kuroga wakiwa njiani kuelekea kwa Babu Ambi huko Loliondo kupata Kikombe.
Mdau Kim na swahiba wake mara baada ya kupata kikombe.
Biashara ya Nyama ya Mbuzi ndio imeshika kasi huko Loli kwa Babu ambi.
Kipini kikiwa kimekomaa ile mbaya kuelekea kwa Babu Ambi.
Hapo bado kama kilomita 40 hivi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. BLOG YETU WOTE, LAKINI UCHUNGUZI YAKINIFU UNAONYESHA KWAMBA ANKAL UNATUTENGA WABEBA BOKSI NA UNAWAPENDELEA WALA VUMBI. MADA ZA WALA VUMBI NYINGI UNAZITUNDIKA LAKINI ZETU SISI WABEBA BOKSI UNAZICHUJA SANA.
    BLOG YETU WOTE, KWANINI UPENDELEE WALA VUMBI?

    NAENDA KUBEBA BOKSI KWANZA, MAANA NAISHI MALMO SWEDEN LAKINI NABEBA BOKSI COPENHAGEN(KOBENHAVEN) DENMARK. NI NCHI MBILI TOFAUTI HIZI, LAKINI UKIVUKA DARAJA TUU USHAINGIA DENMARK.

    MKURUGENZI MKUU MSAIDIZI WA WABEBA BOKSI,
    MALMO, SWEDEN.
    MKURUGENZI MSAIDIZI WA WABEBA BOKSI.
    MALMO, SWEDEN.

    ReplyDelete
  2. ankal naomba niulize maswali machache hapa kuhusu huko loliondo kwa babu ambi..

    nilisoma kwenye vyombo vya habari zaidi ya wiki mbili zilizopita kua wahusika serikalini walichukua sampuli za dawa ya babu pamoja na kuoneshwa utayarishaji wa dawa yenyewe na wakaahidi kua uchunguzi wa kimaabara utafanyika haraka na watu watapewa majibu ya kisayansi kama either dawa inatibu kweli magonjwa hayo sugu, je dawa hiyo ina madhara kwa afya za watumiaji kwa badae (either short term or long term side effects) nk. ila nsikitika hadi sasa watanzania wengi pamoja na viongozi wa serikali wanawaza Loliondo tu huku wengi wakiwa bado hawajui ukweli wa tiba hiyo.

    mimi sipingani na masuala ya kiimani katika maisha ya mwanadam yoyote hivyo basi kama dawa yenyewe inategemea zaidi imani basi Je ni jitihada zipi zimeshafanyika hadi sasa kutoka kwa wahusika wakuu serikalini, madakitari wetu,nk kufuatilia kwa ukaribu watu wanaodai kua wamepona kutokana na dawa hiyo ya babu kwa kutizama mambo kama vile:

    mhussika alikua na ugojwa gani, historia ya ugonjwa wake, kaugua kwa mda gani, medical records za mgonjwa nk kabla hajatumia dawa ya babu, then baada ya kutumia dawa maendeleo yake yamekuaje na umma utangaziwe pamoja na watu kupewa taadhari mbalimbali.

    Pia ninyi waandishi mnahusika kwa kiasi kikubwa kuwafahamisha watu hali halisi, upi ukweli, upi uongo, nk. tangu babu amechukua umaarufu wa kutibu watu waliokwisha kutumia hiyo dawa ni wengi sana ila waandishi wengi wanatuonesha hali halisi ya kwa babu tu kama vile foleni ya magari loliondo,msongamano wa watu na vigogo wanaopata kikombe cha babu,nk. Hali hii ndio inazidi kuwavuta watu wengi zaidi kwenda kujaribu

    kama mnavyowafuatilia wanaokwenda kwa babu, kumhoji babu nk basi ni vyema mkaendeleza uchunguzi kwa wale wanaodai kuponywa na wasioponywa pia pamoja na matatizo yaliyokua yakiwakabili nk hii itakua ni njia nzuri pia ya kuwasaidia wengi wanaobaki kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu hadi sasa.

    Pia ningewaomba hao waliokunywa dawa hiyo, kwa ridhaa yao wafanye vipimo vya uhakika halafu watuhakikishie kua wamepona au la, hii itatupa majibu badala ya kusubiri majibu ya mkemia mkuu wa serikali ( huenda watatoa majibu kuhusu dawa ya babu kama matatizo yatajitokeza).

    Asante

    ReplyDelete
  3. mdau wa pili umeongea point waandishi wa habari wa tanzania uozo tu sijui wamesomea wapi kazi zao ebu auncle angalia documentary ya ntv kenya kuhusu kwa babu the loliondo wonder part 1 and 2. mtangazaji aliyeandaa documentary hiyo unaona kabisa jinsi anavyojua kazi yake sio wenzetu wa tz

    ReplyDelete
  4. ni kweli kabisa nimeingalia hiyo documentary ntv kenya wametengeneza vizuri sana.pia auncle atika hiyo ntv kenya waziri wao wa afya anasema babu wa loliondo afungwe kwa kuwapotosha wananchi na kawashauri wakenya wasiende loliondo huyo waziri wao wa afya naona anatakiwa naye aende akanywe kikombe kwa babu. auncle unatakiwa uweke vitu kama hivyo kwenye blog yako watu wachangie na uakika wengi hawajaona hiyo doumentary ya loliondo wonder na huyo waziri wao anayeongea utumbo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...