Ubalozi wa Tanzania Japan unapenda kuwajulisha kuwa umeendelea kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali ya Japan kuhusu hali inavyoendela kufuatia hitilafu ya mitambo/vinu vya kufua nuklia iliyotokea na inayoendelea kutokea katika mkoa wa Fukushima, pamoja na matetemeko yanayoendelea. Ubalozi umehakikishiwa kwamba bado maeneo mengi ni salama, ukiacha maeneo ambayo yapo umbali wa km 20 kutoka katika mitambo hiyo (exclusive zone) na km 20 hadi 30 ambako watu wamepewa maelekezo ya kukaa ndani.

Aidha, Ubalozi umejulishwa kuwa, pamoja na kwamba mionzi ya nuklia kutoka kwenye vinu hivyo imeweza kusambaa hadi maeneo mengine kama Tokyo, Kanagawa, Kawasaki, Ibaraki n.k., kiwango kilichopo ni kidogo sana kuweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu.

Pamoja na taarifa hizo zilizotolewa na Serikali ya Japan kuwa hali ni salama, Ubalozi unawaomba Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zaidi. Hivyo, unatoa rai kwa Watanzania wote wanaoishi Japan kutoa ushirikiano ili Ubalozi uweze kuweka rekodi zao kwa usahihi (up-date information), ukizingatia kwamba baadhi walisharudi Tanzania, wengine wamehamia katika maeneo mengine na wapo pia waliobadilisha namba zao za simu. Taarifa hizo zitausaidia Ubalozi kufanya mawasiliano ya haraka na kila mtu endapo hali ya kiusalama itakuwa mbaya na kulazimu tahadhari za ziada kuchukuliwa.

Hivyo tunaomba kila Mtanzania atume taarifa zifuatazo kwenye anwani za Ubalozi zitakazotajwa hapo chini.

1. Jina kamili

2. Orodha kamili ya familia yako (kama unaishi na familia)

3. Anwani ya mahali unapoishi (mtaa/mji/eneo n.k.)

4. Namba za simu unazotumia (mobile phone/residential)mawasiliano yake ikiwa ni pamoja na jina, simu/email, anuani ya unapoishi, eneo/mji/mtaa, n.k.

Taarifa hizo zitumwe kwenye e-mail addresses zifuatazo:-

Ubalozi unaomba ushirikiano wenu, na kila upatapo ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako.

Tafadhali tunaomba taarifa hizo zitumwe kwenye anuani pepe zifuatazo

1. jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp

2. fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp

3. tzrepjp@tanzaniaembassy.or.jp

4. tzrepjp@gol.com

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Japan.

16/03/2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Poleni sana Wajapani..

    Ila mbona mnaanza kutafutana/kutambuana katika siku za Matatizo tu??
    Siku zingine mlikuwa mnaishi vp wandugu??

    ReplyDelete
  2. Mimi naishi Japan. sioni haja ya kupeana namba. kama serikali yoyote itayayoweza kunisaidia ni serikali ya Japan sio ya kwetu. Nyinyi mlikaa kimya wakati internet inafanya kazi leo ndio mmeamkaa. Serikali ya tanzania itanipa ticket au chakula an maji? Acheni zenu. Information zote napata katika mji wangu na TV kama nyinyi.

    Mdau Tokyo

    ReplyDelete
  3. Lakini mbona USA wamewaambia raia wao wakae mbali zaidi ya km 50? Hiyo ishirin sijui ...Tokeni huko...Kama unaweza kurudi bongo kwa muda ni heri...Japan hawasemi ukweli mtakuja pata cancer sijui nani atawatibu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...