Kijana wa Miaka 17 Jafar Welino mkazi wa mtaa wa Mianzini Kitongoji cha Mabatini jijini Mbeya ambaye ameibuka na kutoa tiba ya magonjwa sugu kwa mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya na viotongoji vyake.
Mama mkubwa wa kijana huyo,Edina Sanga akiwamiminia dawa wakazi wa jiji la Mbeya
Tangazo husika.
Dogo akipata kikombe
Mama mkubwa wa kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edina Sanga akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii kuwa kijana huyo alianza tiba hiyo wiki mbili zilizopita ambapo kabla ya kuanza kutibu alimueleza mama yake huyo kuwa alitokewa na mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni marehemu akimuelekeza kurithi mikoba yake.
Dawa ikichemka jikoni.
Mdau Rashid Mkwinda akipata maelezo toka kwa waliojitokeza kupata dawa hiyo.
Watu wengi wamejitokeza kupata tiba hiyo.
Picha zote na MbeyaYetu Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Miaka yote ambayo nilikuwa najiuliza ni kwa nini tanzania tuko nyuma kimaendeleo sasa nimepata jawabu: ni kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wake ni wagonjwa!!! hebu ona foleni hapo na kwa yule babu, ikiwa idadi yote hiyo ni wagonjwa ni nani wangapi walio na siha njema ya kuweza kulibeba taifa hili?

    tena kuna suali la kama kweli hii ni tiba au ni kasumba tu!

    Michuzi sijasema baya hapa, kwa hiyo sitegemei kuwekwa kapuni, please!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hapo kazi ipo. Usanii umezidi Tanzania!!!

    ReplyDelete
  3. Haya makubwa kila kukicha aibu zinaziiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. tanzania nchi ya matukio,isiyo na sera zenye kutekelezeka na kupimika kwa viwango vya uwajibikaji.
    mtu mmoja akianzisha biashara ya kuuza kitu flani,kila kona inashamiri hiyohiyo biashara.wakianzisha mashindano ya miss flan,kila kona ya mtaa kunakuwa na mashindano ya miss flan.
    hii ndiyo halihalisi ya nchi ya watu wasio na maono wala mwelekeo.na ukijitokeza na wazo lenye tija linaloweza kubadili maisha, unakuwa wakwanza kupingwa na ikibidi kudhalilishwa na kuitwa kwa majina.
    hii ndiyo nchi yetu TANZANIA.
    SASA NI WIMBI LA KUOTESHWA KUTIBU MAGONJWA SUGU

    ReplyDelete
  5. All this Babu na wengine na vikombe vyao na mizizi iliyochemshwa inanitia hufo sana. All this in my opinion is symptomatic of some serious underlying problems that must for years have been suppressed for some reason. Its easy to pooh pooh as ujinga au upumbavu, I dont think so.Yote hayo yaweza kuitumbukiza nchi kwenye janga kuu. Moyo wangu wauma mno. Serikali ifungue bodi moja kubwa na yenye madaraka ila kuchungua visa hivi kabla havijatuletea machozi ya majuto
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  6. MWAKA HUU TUTAONA MENGI

    ReplyDelete
  7. Nyerere alisema adui wa maendeleo ni umasikini na ujinga ndo hicho kinachoendelea hapo nothing else people are desperate to do anything and everything ili waishi. Mercy me!
    P.S Nibanie na hiyo comment michuzi utani inspire niirudishe Ze utamu ili wadau tutumie freedom of speech yetu

    ReplyDelete
  8. Ilianzia Samunge,Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwaisapile then Tarakea,Rombo kwa Kitwai kabla ya Kamati ya Ulinzi ya wilaya kusitisha utolewaji wa dawa na sasa Mbeya ? Tanzania nchi yenye "amani" na dawa za mitishamba bila kuthibitishwa na mkemia kwa matumizi ya binadamu,ni kuibua ugonjwa mwingine mbali ya umaskini na ujinga.
    Mdau wa USA.

    ReplyDelete
  9. huyu dogo inabidi tuombe watoto wa afande mwema wampeleke kwa babu hajatulia yani anataka kumpiku babu hivi hivi

    ReplyDelete
  10. Sasa usanii unaanza sasa....kama kawaida yetu wabongo. Mtu mmoja akianza tu, wote wanataka hivyo hivyo. Acheni hizo! Hakuna cha tiba hapo wala nini, tufanyeni kazi zetu tuache ujinga, kama unaumwa nenda Hospitali mara moja.

    CHIBI.

    ReplyDelete
  11. Huu ni mwanzo tu. Kina babu watazidi kuwa wengi sana Tanzania kwa kuwa kiwango chetu cha elimu na sayansi ni duni sana na watu wengi wako tayari kuamini 'miujiza' kirahisi sana. Wadau nasikia kuwa yule babu original wa Tegeta/Kunduchi miaka ya 2000-2003 ambaye pia alikuwa anadai anatibu watu 'kimiujiza' amefarikiki dunia. Naomba data zaidi.

    ReplyDelete
  12. Hii inaitwa OIT (only in Tanzania). Licha ya kuwa watu wengi waliokwenda Loliondo hawajapona na wengine wamekufa, bado kuna watu wanakimbilia huko na wapasha habari - hasa tv na magazeti - hawataki kuwaambia wananchi ukweli huo. Inasikitisha lakini ukweli ni kuwa "Welcome to Tanzania, the land of popobawas, albino killers, wachuna ngozi, the old babu and the new babu!!!" Nadhani kaulimbiu hii inaweza kuwavutia watalii wanaotaka kuja kuona watu wenye mawazo ya karne ya kumi wanaishije. Sad, sad, sad....

    ReplyDelete
  13. Please God help this Country this is the way we called desperation. There's no hope at all.God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  14. Mwisho watu watakunywa sumu eti dawa!

    ReplyDelete
  15. -Chinese proverb-

    "Between a fellow who is stupid and honest and one who is smart and crooked, I will take the first. I won’t get much out of him, but with that other guy I can’t keep what I’ve got."

    ReplyDelete
  16. Sasa wale wasiomwamini Mchungaji mmeletewa Mganga wenu. Wale wote wasiopenda kutibiwa na Yesu, nendeni huku. Wanaomwamini Yesu waende Loliondo na wanaoamini Dini zingine nendeni huku Mbeya. Na wale ambao wanaamini Muhimbili tu muelekee muhimbili. Hakuna haja ya malumbano tena.

    ReplyDelete
  17. Kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo :)

    ReplyDelete
  18. naona No2 picha, bibi yuko update anatext uku anamimina dawa

    ReplyDelete
  19. Tanzania ndo tulivyo, ukifungua saloon mwengine anafungua pembeni yako

    ReplyDelete
  20. WATANZANIA WAJINGA SANA SHIDA YETU TULIDUMA TOKA ZAMANI HII NDIO FAIDA YAKE SASA KUWA NA WATU WAJINGA KWA SABABU KIOGOZI ALIKUWA MJINGA ANATOKEA MTU ANASEMA NINA DAWA NA WW UNAKUNYWA HII SI HATARI NAAMINI MUDA MDOGO TUTAPATA MAJIBU JUU YA HIZO DAWA MAAFA MENGINE YANAKUJA

    ReplyDelete
  21. Watanzania tutafakari kabla ya kutenda.hata penye ukweli pataonekana utani kwa sababu ya mengi maigizo.

    ReplyDelete
  22. mimi naona watanzania tungepatiwa vikombe vya kutibu magonjwa sugu kama mtimanyongo , roho ya kwanini na ufisadi

    ReplyDelete
  23. Michuzi tupe raha..Duh! masikini nchi yangu ...Kwanza nilicheka halafu nikaja kaa chini na kufikiria hii si utani ni shida sana ya Tafa...kwa vile serikali wala hajasema chochote kuhusu haya madawa yasiyo na mbele wala nyuma. Watu wasio na la kufikiria au kuelimishwa wanaachiwa waende tu ati kwa vile you don't loose anything ukinywa hiyo dawa au la? You loose a lot...Time, money and you could loose your life too...Is that not something?????

    Halafu tatizo letu lingine bongo twasomea kupasi mitihani tu hatufundishwi critical thinking kabisa ndio maana haya yanatokea sasa. wengi bongo ni waigaji tu hawajui kuvumbua vyao..Ukinunua lory la mizigo kila mtu ataenda nunua, Ona miss so and soo kila mtu miss siku hizi, biashara ya China kila mtu ni china, china china...Hakuna diversity kabisa katika mambo yote bongo. Kuna vitu au services huwezi kuzipata mpaka uende Kenya au SA kukipata, why???? hakuna aliyewaza kuanzisha kitu kingine zaidi ya kusubiri jirani afanye hili na yeye kesho aige...Wasoi wengi lakini wote wanasubiri kuajiriwa tu na hata kama ni mikopo ya biashara hakuna anayefikiria kufanya jambo lingine zaidi ya kuchungulia nani kafanya nini na mimi niige hapo....

    ReplyDelete
  24. mimi langu ni kwamba kama unaweza kupata pesa kwa kutumia akili yako ni nizuri sana. biashara ziko za aina nyingi. if it pays go for it.
    these people are not going around stealing or kiling others so tusaache. waganga wa kienyeji wako kila mahali hata ulaya wako japokuwa wana fancy names kama psychics or seers lakini kazi ni hiyo hiyo.

    ReplyDelete
  25. hata babu anye msanii lakini walisema wachache, na wakazongwa.\

    nyie mnataka babu a monopolize soko?

    ReplyDelete
  26. Incredible. As Tanzanian living in the USA and I warn you I am not a box carrier, I am extremely ashamed of my country. I am ashamed to see that masses are deliberately following these scam bags to no end. Many are going to lose their sacred lives because of following this stupidity. Indeed this is very shameful and discouraging. I blame all this to lack of better education and faith in our God. Stupidity has no limitations...

    ReplyDelete
  27. MMETOA MAPUNGUFU TUUUUUUUUUUUUU YA WATANZANIA.
    1.MBONA HAMSEMI NINI KIFANYIKE?
    2.NANI WA KULAUMIWA KATI YA WANANCHI AU SERIKALI?
    3.JE HAMJUI KWAMBA KUJIDHARAU KWENYE BLOG KAMA HII INAYOSOMWA NA WATU HATA WASIO WATZ NI UDHAIFU MKUBWA AMBAO HATIMA YAKE NI KUMPA ADUI NAFASI YA KUKUMALIZA?

    HAWA WALIOTOA MAONI YA KUJIDHARAU NA KUWADHARAU WATANZANIA BADALA YA KUTOA MAJIBU YA MATATIZO YA WATANZANIA NDIO WAJINGA WALIOPITILIZA AMBAO HATA KAMA BAADHI YAO WAMEBAHATIKA WAKO MAMTONI WANABEBA MABOX WALIPASWA WALETE UJUZI ILI NCHI IENDELEE NA SIO KUUNGANA NA ULIOWAITA WAJINGA.
    ELIMU YETU NI NZURI SANA ILA HAMUITUMII VIZURI KWA SABABU YA KUPENDA KUJIDHARAU NA KUTUKUZA VYA WENGINE. SHAME ON YOU GUYZ.

    ReplyDelete
  28. eti waTZ hatufundishwi critical thinking (CT),we kama ulienda class kusindikiza wenzako, ni wewe, ukafaulu kwa kudesa,unadhani wote.Iloooo, na ushindwe. mangapi tunafanya nakwavile yanathaminiwa na wengine, wanachukuliwa, watz wangapi wapo nje ya nchi na wanategemewa sana na elimu yao walipata Tz, msiwe mnakurupuka, kujidai mnajua kuchonga, mtabaki ivo ivo, ni lini we unayesema hatufundishwi CT,japo meandika maoni katika magazeti viongozi wetu wanayofanya? WaTZ ni simba mwenda pole siku wakiamka, Dunia itashngaa hawakurupuki, nadhani majibu tumeanza kuyaona,acheni dharau,uko mamtoni mpo mnaosha wazee alafu mnajidai hamfundishwi CT,nakwavile mpo nje kwenye sector ya wajinga kama nyie hamjui tunavyothaminiwa, na waTZ wangapi wako katika sector nyeti uko ulaya kwanini msirudi,mkafungua biashara mnazosema,ni vitu gani vipya bongo, na hamnunui wala kuvitumia, nilienda nje,eti mtanzania anashangaa kuona naogea showerGel,kwaaibu anajidai,bongo mnaogea mbuni,nilimuona mshamba,anatoka kijijini TZ,akifika nje kila kitu anaona kipya.Acheni kutudharau,mjidharau wenyewe msiojua kinachoendelea nchini na msiokua na Busara kitu gani hakipo bongo.Tunauwezo wakufungua hospitali kubwa kama tunazozifuata uko india, lakini viongozi ndo wanakwamisha. saweunageneralize eti waTZ not CT, wewe ndo ivo, juice ya upupu umekunywa nadhani. Fikra zenu ndo za kale,w2 nje wanatamanikurudi kwenye iyo mitishamba lakini wamebanwa kweli,na pamoja izo technologia bado, madawa yao ni ovyo,na cancer kibao.Ovyoooooooooooooooo!!!!!!!

    ReplyDelete
  29. kipindi chote alikuwa wapi aache uzushi

    ReplyDelete
  30. we mdau sun marc 27, 01:54;pm, we jidanganye hivyo hivyo kweli naunga mkono bongo watu hawafundishwi ct maana unaona hata rais wetu baada ya kupeleka wataalam na kuichukua sample na kuhakikisha kama kweli inatib hiyo dawa akaanza mwenyewe kunywa , na bongo itabak bongo tu na mamton ni mamton kwa oppotunity, na ukianza kuzungumzia cancer sasa hiv hapa inatibiwa na unapona kama inaanza sasa we jidanganye na maendeleo ya ufisad, bidhaa mbov kutoka china ,umeme wa dowans ,huku mambo mswano we utabakia la labda tu na kila kukicha kusema watu wanosha vibibi lakin wana security na unaishi na matumain,watanzania tuache kukimbilia mambo lazima tujiulize si kujinywea mizizi tu ambayo hata haijathibitishwa kama ni dawa au sumu ,MICHUZI ISIIIBANIE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...